BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATANO TAREHE 04-01-2020

Manchester United wanajiandaa kutangaza dau la kumnunua beki wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 20, huku kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, akiwa tayari kuondoka Old Trafford. (Star)
Mashetaniwekundu hueda wakalazimika kumlipa mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 31, ada ya kila mwaka ya £1.1m atakaporejea kutoka Inter Milan ambako amekuwa akicheza kwa mkopo. (Sun)
Everton wanapanga kuweka dau kubwa la kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 30, msimu wa joto pamoja na kiungo wa kati wa Juventus Aaron Ramsey, 29. (90min.com)
Kwa sasa, the Toffees wanatumia huduma ya mawasiliano ya kidigitali ya Zoom inayowakutanisha kwa njia ya video wachezaji na wahudumu wa afya wa klabu hiyo, huku kiungo wa kati wa Ufaransa aliyejeruhiwa Schneiderlin, 30, akijiandaa kuzungumza na mtaalamu wake wa upasuaji kupitia mfumo huo. (Guardian)
PogbaHaki miliki ya pichan
Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema, 32, ametetea kauli yake baada ya kumfananisha mshambuliaji wa Chelsea na mchezaji mwenza wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, 33, 'gari dogo linaloenda kasi lakini halina nguvu'alipofanya Instagram live. (Marca)
Arsenal wanawataka ndugu wawili wa Ivory Coast, Hamed Traore, 20, kiungo wa kati ambaye yuko Sassuolo kwa mkopo kutoka Empoli, na ndugu yake Amad, 17, ambaye ni winga wa Atalanta. (90min.com)
Liverpool hawana mpango wa kumsajili tena kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 27, ambaye yuko Bayern Munich kwa mkopo kutoka Barcelona. (Mirror)
Manchester United wameelekeza darubini yao kwa kiungo wa kati wa Leicester City na England James Maddison, 23, baada ya nahodha wa Aston Villa Jack Grealish, 24, ambaye wamekuwa wakimnyatia kwa
muda mrefu kuhusishwa na kisa cha utata nje ya uwanja. (Daily Star)
Liverpool hawana mpango wa kumsajili tena kiungo wa kati wa Brazil Philippe CoutinhoHaki miliki ya pichan
Real Madrid wanamfuatilia karibu nyota wa Sao Paulo Igor Gomes, 21, maarufu 'Kaka mpya' huku Barcelona, Sevilla na Ajax pia wakimng'ang'ania mchezaji huyo wa safu ya kati ya Brazili wa chini ya miaka 20. (AS)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 31, amedokeza kuwa ataendelea kucheza katika Ligi Kuu ya soka ya England endapo ataondoka Stamford Bridge, hatua ambayo huenda ikafufua matumaini ya
Arsenal na Tottenham kumsaka. (ESPN Brazil - in Portuguese

Post a Comment

0 Comments