BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAPILI TAREHE 19-04-2020

Borussia Dortmund itamuongezea mshahara wa euro milioni 4 (£3.5m) winga wa Uingereza Jadon Sancho, 20, ikiwa atakataa ombi la kuhamia kwenye ligi ya primia. (Bild, via Mirror)
Newcastle huenda ikaonesha wazi nia yake ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Chile na mchezaji wa Barcelona Arturo Vidal, 32. Mchezaji huyo inasemekana kwamba yuko tayari kuhama ikiwapo timu ya The Magpies itabadilisha kocha wa sasa Steve Bruce na mahala pake kuchukuliwa na Max Allegri. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mshambuliaji wa Uhispania Pablo Mari, 26, anataka kufanya makubaliano yake ya uhamisho wa mkopo kwa Arsenal kutoka Flamengo kuwa wa kudumu msimu ujao. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa France Kylian Mbappe, 21, thamani yake itapungua hadi euro milioni 35 kutoka 40 baada ya virusi vya corona. (AS)
MariHaki miliki ya picha
Arsenal na Everton ziko tayari kumsajili mshambuliaji wa Celtic raia wa Ufaransa Odsonne Edouard, 22. (Le10 Sport - in French)
Arsenal imewasiliana na Reims kwasababu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Ufaransa Axel Disasi, 22. (Goal)
Liverpool imeelekeza macho yake kwa kiungo wa kati wa Inter Milan na Croatia Marcelo Brozovic, 27. (Libero, via Mirror)
Hatahivyo, Liverpool haijawasiliana na RB Leipzig kuhusiana na uhamisho wa mshambuliaji wa Ujerumani, 24, Timo Werner. (General Anzeiger - in German)
Mbappen
Barcelona inataka kumuuza winga wa Brazil Philippe Coutinho - ambaye kwasasa yuko kwa mkopo Bayern Munich - kukiwa na matumiani kwamba kutapatikana mnunuzi anayemuhitaji mchezaji huyo, 27, kutoka ligi ya Primia. (Goal)
Liverpool itapunguza gharama ya winga wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 28, kwasababu ya janga la virusi vya corona. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane huenda akahamia Real Madrid, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa Senegal Keita Balde, ambaye pia aliongeza kuwa Mane, 28, Pia anaweza kusalia Anfield "milele". (AS, in Spanish)
Barcelona inatarajiwa kuwasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 28, kutoka Paris St-Germain.
Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane(Aliye na mpira) huenda akahamia Real MadridHaki miliki ya pichan
Miamba hao wa soka wa Uhispania wako tayari kuwajumuisha Samuel Umtiti, Ousmane Dembele na Jean-Clair Todibo katika mkataba huo baada ya hali yao ya kifedha kuathiriwa na Jana la coronavirus. (Mundo Deportivo, in Spanish)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya Manchester United na huenda akawa kiongozi wa klabu hiyo, kwa mujibu wa mwandishi wa michezo wa Uhispania Guillem Balague. (Express)
Kipa wa muda mrefu wa Juventus Gianluigi Buffon, 42, amekubali kurefusha mkataba wake katika klabu hiyo. Hii itakuwa msimu wa 19 kwa mtaliano huyo Turin. (Tuttosport, in Italian)

Post a Comment

0 Comments