BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAPILI TAREHE 5-4-2020

Arsenal wanaimani kubwa ya kufikia makubaliano ya kumsajili winga wa Bournemouth, Ryan Fraser, 26, mkataba wake utakapomalizika msimu huu. (Teamtalk)
Arsenal huenda ikajaribu kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard, 27, kabla ya msimu ujao, hususan ikiwa mpango wa kuhama kwa mkopo wa kiungo wa kati mwenzake Dani Ceballos, 23, kuelekea The Gunners kutoka Real Madrid hautakuwa wa kudumu. (The Athletic, subscription required)
Hatua ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho, 20, kukataa ombi la kusajiliwa na Chelsea msimu huu, huenda ikawa fursa kwa mchezaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, kuhamia Stamford Bridge. (Sport, in Spanish)
Kocha wa Uingereza Gareth Southgate amekubali kupunguziwa mshahara kwa asilimia 30. (Sky Sports).Haki miliki ya pichaS
Kocha wa Uingereza Gareth Southgate amekubali kupunguziwa mshahara kwa asilimia 30. (Sky Sports).
Mshambuliaji wa Leicester Islam Slimani, 31, anahusishwa na kuhamia Sporting Lisbon baada ya mchezo wake kushindwa kuiridhisha Foxes. (O Jogo, via Leicester Mercury)
Wakati huohuo, Leicester imeonesha nia ya kumsajili mlinzi wa Fenerbahce, Hasan Ali Kaldırım, 30, lakini itapata upinzani kutoka kwa Galatasaray. (Hurriyet, in Turkish)
Aliyekuwa mshambuliaji wa Leeds United, Noel Whelan ameisihi klabu hiyo kumuuza kwa mkopo msimu ujao mshambuliaji mwenye uwezo wa kutegemewa siku zijazo, Ryan Edmondson, 18. (Football Insider)
kennyHaki miliki ya pichaS
Mlinzi wa Everton Jonjoe Kenny, 23, anataka kusalia Schalke msimu ujao baada ya kufurahia uhamisho wake wa mkopo huko Bundesliga. (Bild, in German)
Rangers tayari imeshawatambua wale ambao huenda wakachukua nafasi ya mshambuliaji Alfredo Morelos, 23, ambaye anawaniwa na vilabu kadhaa vya Ulaya. (Goal, in Spanish)
Winga wa Everton Bernard, 27, ametupilia mbali madai ya kwamba kuna uwezekano akahamia klabu ya Italia ya Roma msimu huu. (Liverpool Echo).
West Ham imeungana na wengine katika kinyanganyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani timu ya Freiburg Robin Koch, 23. (Daily Star).
Newcastle itajitahidi kumsajili tena kiungo wa Lille, Boubakary Soumare, 21, baada ya kuonesha nia yao Januari mwaka huu. (Sport, in Spanish).

Post a Comment

0 Comments