BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO IJUMAA TAREHE 03-04-2020

Mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson, 28, amesema hastahili kuhusishwa na ligi kubwa kama ya England kutokana na namna uchezaji wake duni msimu huu. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Gent na Canada Jonathan David, 20, amekiri kuwa angelipendelea kucheza soka ya Ligi ya Primia siku zijazo. (Guardian)
Pierre-Emerick Aubameyang, 30, mshambulliaji wa Arsenal na pamoja na winga wa Manchester City Leroy Sane, 24, ni miongoni mwa wachezaji wanaoumiza vichwa klabu kuhusu kurefushwa kwa mikataba yao baada ya ratiba ya dirisha la uhamisho kusongezwa mbele. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Wolves na Mexico Raul Jimenez, 28, amedokeza kuwa hawezi kuodoka klabu hiyo kutokana na masharti ya mkataba wake licha ya Manchester United na Real Madrid kuonesha ishara ya kutaka kumsajili. (Marca, via Mail)
Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya pichan
Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 23, amejumuishwa katika orodha ya wachezaji wa ziada wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni ya Real Madrid, kutoa nafasi kwa Arsenal kumnunua. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Aston Villa muingereza Jack Grealish, 24, amefahamishwa kuwa hana nafasi ya kujiunga na Manchester United msimu huu. (Star)
Kwengineko, Aston Villa wamehusishwa na kiungo wa kati wa Marseille wa miaka 22- mfaransa Maxime Lopez. (Birmingham Live)
Mshambuliaji wa Tottenham na Korea Kusini Son Heung-min, 27, anajiandaa kufanya huduma ya umma kwa taifa kwa muda wa wiki nne nchini mwake wakati huu ambapo msimu umeahirishwa kutokana na janga la corona. (Sun)
CeballosHaki miliki ya pichan
Mchezaji wa safu ya kati ya Manchester City na Ubelgiji Kevin de Bruyne, 28, ameonya wasimamizi wa klabu hiyo kutokimbilia kuwaregesha uwanjani wachezaji waliojeruhiwa. (Telegraph)
Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti ana hamu sana ya kuungana tena mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez,28, baada ya kuwa mkufunzi wake wakati alipokuwa msimamizi wa miamba hao wa Uhipania. (Mirror)

Post a Comment

0 Comments