BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMIS TAREHE 9-04-2020


Chelsea wapo katika mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa Barcelona na Brazili Philippe Coutinho, 27. Nyota huyo wa zamani wa Liverpool kwa sasa yupo kwa mkopo Bayern Munich. (Sport)
Klabu za Manchester United na Napoli zinataka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 28. (AS, in Spanish)
Kiungo wa Aston Villa na England Jack Grealish, 24, ni moja ya kipaumbele cha usajili wa Manchester United. (Evening Standard)
Nyota wa Aston Villa Jack GrealishHaki miliki ya picha
Barcelona wametupilia mbali nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Brazil Willian,31, japo atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu. (Sport)
Wakati huohuo Chelsea wamefungua mazungumzo na beki wake Mjerumani Antonio Rudiger, 27, ili asaini mkataba utakaombakiza klabuni hapo hadi walau mwaka 2023. (Sky Sports)
Napoli wanataka kumsajili winga wa West Ham na Brazil Felipe Anderson, 26. (Corriere dello Sport, in Italian)
Beki wa Mjerumani Antonio RudigerHaki miliki ya pichan
Klabu ya Besiktas ya Uturuki inapanga kumsajili kipa wa zamani wa timu ya taifa ya England aliyepo klabu ya Burnley kwa sasa, Joe Hart, 32, kama mbadala wa kipa Mjerumani Loris Karius, ambaye anawatumikia kwa mkopo akitokea Liverpool.(Fanatik, in Turkish)
Brighton wanakaribia kumsajili kiungo wa Sydney FC na timu ya taifa ya Australia ya chini ya miaka 17 Cameron Peupion, 17. (Sydney Morning Herald)
Beki Diego Carlos, 27, anasema anafuraha kuwepo katika klabu ya Sevilla licha ya kutakiwa na Liverpool. (Estadio Deportivo, in Spanish)
Nyota wa Liverpool Sadio ManeHaki miliki ya picha
Sadio Mane, 27, anasema alifikiria kujiunga na Manchester United kabla ya kuhamia Liverpool. (Times, subscription required)

Post a Comment

0 Comments