BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA WASIPOKUWA MAKINI WATAMSAHAU SHIBOUBKiungo fundi wa Simba Sharaff Elden Shiboub raia wa Sudan alianza maisha vyema kunako mabingwa hao wa nchiWakati wa kocha Patrick Aussems, Shiboub alijihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza

Lakini tangu timu hiyo ikabidhiwe kwa Sven Vandenbroeck, fundi huyo wa mpira amepoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza.Shiboub amekuwa na nafasi finyu ya kucheza na wakati mwingine huwa anakosekana hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba

Pamoja na ushindani mkubwa wa namba kwenye kikosi cha Simba, lakini Msudan huyo anaamini anastahili kupewa nafasiInaelezwa Shiboub ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao iko ukingoni lakini anasuasua kuongeza mkataba mwingine

Klabu ya El Hilal aliyokuwa akiitumikia imeingia kwenye vita ya kumuwania nyota huyo ambaye ni tegemeo kwa timu ya Taifa ya Sudan.Pia inaelezwa Shiboub ana ofa kutoka nchi za Misri na Afrika Kusini

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema Shiboub ni miongoni mwa wachezaji ambao wako kwenye mchakato wa kuwaongeza mkataba na hawana mpango wa kumuacha

Post a Comment

0 Comments