BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA NA AZAM MAMBO SAFI YANGA NA WENGINE 17 MAJANGA TU



Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (SPOTANZA), Mussa Kisoky, amesema msimu huu wamepokea madai mengi kutoka kwa wachezaji ya kutolipwa fedha za usajili na mahitaji mengine.

Kisoky amesema klabu nyingi zinadaiwa na wachezaji wao isipokuwa Simba na Azam
Amesema hadi sasa hawajapokea kesi yoyote kutoka kwa wachezaji wa Simba na Azam wakilalamikia kutolipwa stahili zao, hivyo kukwepa mtego wa kunyimwa leseni ya kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

"Tatujapata malalamiko kutoka kwa wachezaji wa Azam na Simba msimu huu, nachukua nafasi hii kuzipongeza kwa kujali maslahi ya wafanyakazi wao wanapowasajili au kuvunja nao mikataba," alisema Kisoky.

Alisema kama klabu hizo hazidaiwi na wachezaji wao zitakuwa zimetimiza vigezo vya kupatiwa leseni ya kushiriki michuano inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Kisoky amesema kwa asilimia 80 wamepokea kesi mbalimbali kutoka kwa wachezaji, wakiwamo wa Yanga, Lipuli, Biashara United na nyingine.

Kisoky alisema klabu zinaingia katika madeni makubwa na wachezaji kutokana na utaratibu mbovu wa kuwaacha, jambo ambalo TFF wanatakiwa kuliangalia upya.

"Kumekuwa na utaratibu wa kumwacha mchezaji siku chache kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili na wachezaji kukukubali kusajiliwa timu yoyote ili kulinda viwango vyao wakati huo wakiwa wanadai walikotoka,” alisema Kisoky.

Hivi karibuni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPBL), Almas Kasongo, alisema kuanzia msimu ujao hawatatoa leseni ya kushiriki ligi kwa klabu ambayo itakuwa inadaiwa na wafanyakazi, wachezaji na benchi la ufundi

Post a Comment

0 Comments