BETI NASI UTAJIRIKE

SENZO AFUNGUKA TETESI ZA USAJILI SIMBA


Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema michakato yote ya usajili wa timu hiyo itakamilika mwishoni mwa msimu hivyo mpaka sasa hakuna mchezaji yeyote ambaye ametangazwa kuachwa

Senzo amesema taarifa zote zinazohusiana na usajili litafahamika baada ya msimu kumalizika

"Simba inawachezaji 29 na wachezaji wote ni muhimu sana kwenye timu yetu na mikataba ya baadhi ya wachezaji inaisha mwezi wa Juni lakini wengine wanamikataba mirefu. Kwa sasa si sawa kuzungumzia kuhusu usajili kwamba huyu na huyu wataondoka," amesema

"Kwa sasa tunaangalia mwisho wa msimu tutakuwa na maamuzi, mimi siangalii kinachosemwa kwenye magazeti kwa sababu wao wapo kwa ajili ya kuuza habari mara Deo Kanda anakwenda kule na Dilunga hivyohivyo"

"Kutokana na hilo, taarifa rasmi zitatoka kwenye klabu za wachezaji wote ambao mikataba yao inamalizika tutatoa taarifa mwishoni mwa mwezi wa sita"

"Kwa sasa tunaangalia kuhusu janga la ugonjwa wa Corona, tuna michezo 10 bado hatujacheza kwa hiyo hatupo kwenye kuangalia mambo ya usajili. Tunaangalia zaidi hili janga linalotukabili kwa sasa"

Post a Comment

1 Comments