BETI NASI UTAJIRIKE

NIYONZIMA AMTABIRIA MAKUBWA BALAMA MAPINDUZI



Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima ameeleza kuvutiwa na uchezaji wa kiungo anayecheza nae kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria, Mapinduzi Balama.Niyonzima aliyerejea Yanga mwezi Januari, amesema Balama ni mmoja wa wachezaji bora aliowahi kucheza nao

"Navutiwa sana na uchezaji wa Mapinduzi Balama. Nafikiri akiendelea kujituma atapata mafanikio makubwa sana. Ni mchezji mwenye kipaji na anapokuwa uwanjani anafahamu vyema majukumu yake," amesema Niyonzima

Niyonzima aliongeza kuwa bao alilofunga nyota huyo kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Simba Januari 04 mwaka huu, ni miongoni mwa mabao bora yaliyofungwa msimu huu
Balama aliyetua Yanga mwanzoni mwa msimu akitokea klabu ya Alliance Fc, ameanza vyema maisha yake Jangwani akijihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza licha ya mabadiliko ya makocha watatu

Kiwango chake kimempa nafasi ya kuitwa kikosi cha timu ya Taifa kilichopaswa kushiriki michuano ya CHAN nchini Cameroon ambayo hata hivyo iliahirishwa kutokana na janga la Corona

Post a Comment

0 Comments