BETI NASI UTAJIRIKE

MKUDE AFUNGUKA ATHARI ZA CORONA KWA WACHEZAJI


Kiungo wa Simba Jonas Mkude amesema kuwa endapo Ligi Kuu Bara itaendelea baada ya muda wa kusimama, kutakuwa na changamoto mbalimbali kwa wachezaji kurejea kwenye ari ya mchezo ikiwamo suala la kukosa pumzi na majeraha

Mkude ametoa kauli hiyo wakati huu kukiwa bado haifahamiki ni lini ligi itarejea kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Corona

Fundi huyo wa mpira amesema changamoto kubwa anayoiona iwapo wachezaji watarejea ni kwamba wengi wao watakabiliwa na suala la uwiano tofauti wa pumzi ikiwamo baadhi yao kukata mapema, jambo ambalo litaziathiri timu nyingi katika juhudi za kusaka ushindi.

Aidha, Mkude aliongeza kuwa kutokana na kila mtu kufanya mazoezi kivyake haamini kama kila mmoja anajibidiisha kuyafanya ipasavyo huko aliko kwa sasa.

Ligi mbalimbali za soka duniani zimesimama kupisha juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa corona ambao umekuwa changamoto na kusababisha mambo mengi kusimama.

Post a Comment

0 Comments