BETI NASI UTAJIRIKE

ZAHERA AFUNGUKA HATMA YA MOLINGA YANGABaada ya Yanga kuanza mchakato wa kumrejesha mshambuliaji Heritier Makambo, ni wazi safari ya David Molinga itakuwa imefika tamatiPamoja na kuwa kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga akiwa amefunga mabao nane, Molinga ameshindwa kuwashawishi mashabiki kutokana na kiwango chake kutotabirika

Aidha nidhamu yake inatajwa kumponza zaidi Mcongoman huyo aliyetua Yanga kwa mkopo
Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye ndiye aliyefanikisha usajili wake, amesema Molinga amepata timu na ataondoka mwishoni mwa msimu

"Haonekani kuwa na furaha Yanga, ameniambia amepata timu nyingine hivyo ataondoka mkataba wake ukimalizika," alifichua Zahera ambaye ameweka makazi yake nchini

Mwanzoni mwa msimu Zahera alimtabiria Molinga kuwa atafunga zaidi ya mabao 15 kwenye ligi na kama yasipotimia pasi akatwe mkono

Ni wazi Molinga hataweza kufikisha idadi hiyo ya mabao pengine Zahera ajiandae kukatwa mkono! pamoja na ahadi ya Tsh Milioni 2 ambayo pia aliitoa kwa mmoja wa waandishi wa habari

Post a Comment

0 Comments