BETI NASI UTAJIRIKE

HUYU DOGO ANAYEKUJA JANGWANI NI ZAIDI YA MORRISON


Baada ya usajili wa Bernard Morrison aliyetokea DC Motema Pembe 'kubamba', inaelezwa Yanga inamnyemelea mchezaji kutoka klabu ya AS Vita ya huko DR Congo.Winga Tuisila Kisinda ndiye anayetajwa kutakiwa na mabingwa hao wa kihistoria ukiwa ni mkakati wa kuisuka upya Yanga ya mataji

Nyota huyo ni miongoni mwa waliopendekezwa na kocha Luc Eymaael katika kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.Kisinda ni mmoja wa wachezaji mahiri wa klabu ya AS Vita. Nyota huyo pia anamudu kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati

GSM ndio inayoipa jeuri Yanga wakati huu, inaelezwa wametenga kitita cha Tsh Bilioni 1.5 kwa ajili ya usajili.Nyota wanne wa kigeni watasajiliwa ambapo Eymael tayari amewasilisha mapendekezo yake

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema katika usajili ujao wako tayari kutumia hata dola laki tano kumnasa mchezaji yeyote aliyependekezwa na Eymael

Post a Comment

0 Comments