BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WAJIPANGA KUKABILIANA NA HUJUMA MECHI NA SIMBA


Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wataongeza ulinzi kuelekea kwenye mechi yao ya Simba inayotarajiwa kufanyika Machi 8 Uwanja wa Taifa.Bumbuli amesema kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuongeza usalama na kutunza siri zao kabla ya kukutana na watani zao wa jadi.

"Tunatambua kwamba kuna kazi ngumu ambayo ipo mbele yetu lakini tumejipanga na tulichokifanya kwa sasa ni kuongeza ulinzi ndani ya timu ili kukwepa yale mambo yasiyo ya kitimu kufanyIka kwetu.

"Morali ya wachezaji ni kubwa na kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.

Yanga iliyo chini ya Luc Eymael itakutana Simba iliyotoka kushinda mabao 3-2 mbele ya Azam FC huku wao wakiibamiza Mbao FC mabao 2-0 zote zilicheza Uwanja wa Taifa.

Post a Comment

0 Comments