BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WAJA NA MBINU MPYA ZA KUIFUNGA SIMBA
mabosi wa Yanga wameamua kumkabidhi majukumu ya kukisuka kikosi kitakachoimaliza Simba, Machi 8 Uwanja wa Taifa Kocha Msaidizi wa timu hiyyo Charles Mkwasa.

Simba itakaribishwa na Yanga Machi 8 Uwanja wa Taifa wakiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2.

Habari zinaeleza kuwa tayari jukumu la kukipanga kikosi kitakachoimaliza Simba lipo mkononi mwa Mkwassa ambaye aliimaliza Simba walipokutana nayo mchezo wa mzunguko wa kwanza.

"Simba wanajua itakuwa kazi rahisi kwa kuwa wanatambua kwamba Kocha Mkuu Luc Eymael hawatambui, kilichokubaliwa kwa sasa ni kuona majukumu yote kuhusu Simba, Mkwassa anayafanya.

"Kwenye ile sare ya mabao 2-2 Mkwassa ndiyo alikuwa shujaa sasa mchezo wetu unaofuata ni lazima pia tumpate shujaa wa mara ya pili," ilieleza taaarifa hiyo.

Eymael amesema kuwa wanachokifanya benchi la ufundi ni kufanya kazi kwa kushirikiana.

Post a Comment

0 Comments