BETI NASI UTAJIRIKE

WAWA AFUNGUKA ANAYOYAFANYA KIPINDI HIKI CHA LIGI KUSIMAMA



Beki wa Simba Pascal Wawa amesema kuwa kwa sasa yupo salama na anaendelea kufanya mazoezi binafsi ili kulinda kipaji chake huku akitumia muda mwingi kucheza gemu na kufanya mazoezi binafsi.

Wawa,kwenye mabao 63 ya Simba amehusika kwa kutoa pasi moja ya bao, akimpa Meddie Kagere, amesema  kuwa analinda uwezo wake kwa wakati huu ambao Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali ili kupambana na Virusi vya Corona.

Nipo salama kwa sasa ninamshukuru Mungu, nashinda mwenyewe nyumbani nikiendelea kujiweka fiti ambapo ninatumia muda mwingi kufanya mazoezi mepesi binafsi ikiwa ni pamoja na kupiga pushapu, pia ninapenda kucheza gemu ili kuwa bora,” amesema.

Safu ya ulinzi ya Simba iliyo chini ya Wawa imeruhusu kufungwa mabao 15 kwenye mechi 28 walizocheza sawa na dakika 2,520 ikiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 168.

Post a Comment

0 Comments