BETI NASI UTAJIRIKE

VIRUSI VYA CORONA : WAZIRI MKUU JAPANI AZUA TAHARUKI KUAHIRISHA OLYMPICSWakati dunia nzima ikihangaika kuahirisha michuano ya Olympics 2020kutokana na kusambaa kwa virusi vya COVID 19 waziri mkuu wa Japan hana mpango wa kuahirisha michuano hiyo inayotakiwa kuanza mwezi julai 24.

Mbali na kukumbwa na visa 847 huku watu 28 wakifariki kutokana na Corona lakini waziri mkuu Shinzo Abe amenukuliwa akisema 

"Tuna sapoti kutoka G7 kwamba Tokyo Olympic na Paralympic itaruhusiwa kama ushindi wa binadamu dhidi ya virusi vya Corona .

"Tutakutana na kamati za International Olympic Committee pamoja na World Health Organization na kujua ni jinsi gani tutafanikisha michezo hiyo"

Kama hali itakuwa shwari mpaka mwezi wa sita mwishoni basi michuano hiyo inaweza kufanyika. Endapo haliikiwa ni tofauti basi michuano hiyo itaahirishwa na kupanga kwa wkati mwingine.

Post a Comment

0 Comments