BETI NASI UTAJIRIKE

DR MSOLA AJA NA MBINU MPYA YA KUIFUNGA SIMBA JUMAPILI


Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wake kuwa na mshikamano kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Taifa Jumapili ijayo

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema viongozi wanatimiza wajibu wao kuhakikisha wachezaji wanapata kila kitu kwenye maandalizi yao huku akiwataka mashabiki na wadau wa Yanga kuungana nao katika kuhakikisha wanashinda mchezo huo

"Uongozi unajitahidi kutimiza majukumu yake ili kuhakikisha timu inakuwa na mazingira mazuri. Hivi sasa Tumeweka utaratibu wa kuzungumza na wachezaji pamoja na benchi la ufundi kwa nyakati tofauti kuhakikisha kila kitu kiko sawa kuelekea mchezo huo na michezo mingine itakayofuata"
"Lakini hili sio la viongozi pekee, nadhani Wanayanga wote tunatakiwa kushikamana kila mmoja na nafasi na uwezo wake ili kuhakikisha tunashinda mchezo huo. Naamini kwa ushirikiano wetu kama Wanayanga, tunaweza kushinda na kila mmoja wetu kufurahi"

Naye aliyewahi kuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabuni hapo, Jerry Muro, amesema wanayanga wanapaswa kuwa wamoja ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo

"Kama una chuki labda na kiongozi, ni vyema kuacha kwani huu sio muda wake, ni wakati wa kushirikiana na kuongeza nguvu kwenye timu"
Muro ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, aliwataka wapenzi wa Yanga kuwa kitu kimoja na kila mmoja kutoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha Simba inafungwa Jumapili.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga, Hassan Bumbuli amesema mchezo huu ni wa Wanayanga wote kwani matokeo ya ushindi yatafurahiwa na kila mmoja
"Yanga si timu ya mtu mmoja au kundi fulani la watu, kila mwenye mapenzi na klabu hii, atoe mchango wake ili tuweze kupeleka ‘msiba’ Msimbazi Jumapili kwani sababu, nia na uwezo wa kufanya hivyo tunao kutokana na ubora wa wachezaji wetu na benchi la ufundi"

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo uliopigwa Januari 4, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Yanga iliwashangaza wengi baada ya kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2.

Kilichowavutia zaidi Wanayanga, ni kitendo cha kufunga mabao yote mawili ndani ya dakika tatu, likiwamo moja la ‘kuombea mkopo benki’ lililofungwa na Mapinduzi Balama.
Yanga wataingia uwanjani Jumapili huku wakifahamu wazi ushindi utakuwa na maana kubwa kwao

Post a Comment

0 Comments