BETI NASI UTAJIRIKE

GSM HII SASA SIFA,WAMFUNIKA MO DEWJI KWA KUMWAGA MAMILIONI


Uongozi wa klabu ya Yanga umetaka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili, March 08 kwenye uwanja wa Taifa.Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema timu inaendelea na maandalizi yake kuelekea mchezo huo

Amesema wote wako katika hali nzuri ispokuwa winga Juma Mahadhi ambaye ameanza mazoezi hivi karibuni baada ya kupona majeraha ya goti yaliyomuweka nje kwa zaidi ya mwaka mmoja

"Wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo isipokuwa Juma Mahadhi ambaye bado hayuko sawa kiafya"

"Tunawataka mashabiki waje kwa wingi watuunge mkono katika mchezo huu ambao sisi ni wenyeji. Wakifika uwanjani waanze kukaa majukwa ambayo wapinzani wetu hukaa kwani huu ni mchezo wetu, tunaweza kujipangia utaratibu wa kukaa tunaotaka," amesema

Aidha Bumbuli amesema kuelekea mchezo huo Yanga hawatahamisha kambi yao iliyopo Regency Hotel, pia wataendelea kufanya mazoezi yao viwanja vya Chuo cha Sheria, jambo kubwa walilofanya ni kuongeza ulinzi

GSM kutoa Milioni 200 

Katika hatua nyingine, GSM wameahidi kutoa kitita cha Tsh Milioni 200 za hamasa ili Yanga iweze kushinda
Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz amethibitisha kuwa ahadi hiyo tayari imewasilishwa na wadhamini wao hao wanaohusika na kutengeneza na kusambaza jezi za klabu ya Yanga

Kwa upande wa Simba inasemekana Mo Dewji ameahidi bonasi ya milioni 100 kwa wachezaji na benchi la ufundi endapo tu watashinda mchezo huo.


Post a Comment

0 Comments