BETI NASI UTAJIRIKE

UCHAMBUZI: KIPI KIMEMKUMBA DOUGLAS MUNISHI "DIDA" NDANI YA LIPULI?


Maisha mapya ndani ya Lipuli kwa Deogratius Munish bado hayajakaa sawa kwenye mechi zake alizokaa langoni ameshindwa kuondoka langoni bila kufungwa.
Mechi 8 alizokaa langoni amefungwa mabao 16 timu yake imefunga mabao nane, kwenye pointi 24 walizokuwa wakizisaka Lipuli wamevuna pointi mbili baada ya kulazimisha sare mechi mbili na kuziyeyusha pointi 22.
Dida ana wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 45 jambo ambalo limekuwa likimuumiza kipa huyo aliyewahi kuitumikia Yanga na Simba ambapo amesajiliwa na Lipuli akiwa mchezaji huru.
Mechi zake ilikuwa ni mbele ya :-Ruvu Shooting 3-1 Lipuli, Februari 20, Yanga 2-1 Lipuli, Februari 5, Lipuli 1-1 JKT Tanzania Februari 11,Mbeya City 2-1 Lipuli, Februari 18, Tanzania Prisons 2-0 Lipuli, Februari 23, Lipuli 1-2 Namungo , Februari 29, Lipuli 3-3 Ndanda, Machi 3, Machi 10, Lipuli 0-1 Kagera Sugar.
 Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha mambukizi ya Virusi vya Corona.

Post a Comment

0 Comments