BETI NASI UTAJIRIKE

MAGORI AYAPINGA MAAMUZI YA BODI YA LIGI



Uamuzi wa kutangaza uwezekano wa kucheza mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara bila ya kuhudhuriwa na mashabiki umeelezwa kutolewa kwa haraka kabla ya kusubiri taarifa za maendeleo ya kuhusiana na hali ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona (COVID 19), ambayo yameingia nchini

Ikiwa imepita siku moja baada ya serikali kusimamisha shughuli mbalimbali za mikusanyiko, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia Kamati ya Bodi ya Ligi Nchini (TPLB), juzi lilitangaza mechi za Ligi Kuu Bara zinaweza kuendelea lakini bila ya mashabiki ili kukamilisha msimu wa 2019/2020.

Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba, Crescentius Magori, amesema uamuzi huo ulitolewa kwa makosa na Bodi ya Ligi ilipaswa kusubiri kupokea taarifa kuhusiana na hali ya maambukizi baada ya kupita wiki mbili au tatu.

Magori alisema kutangaza kuendelea na mechi za ligi mbalimbali bila mashabiki kwa sasa haikuwa sahihi kwa sababu huenda hali ya maambukizi inaweza kuwa mbaya zaidi na hivyo kuathiri wachezaji na viongozi watakaosimamia michezo hiyo.

"Ni uamuzi wa haraka, huwezi kujua huko mbele hali itakuwaje, huenda ikadhibitiwa mapema na hali ikarejea sawa sawa au hali ikawa mbaya zaidi hata kuchezwa bila mashabiki haiwezekani, nashauri tathmini ingefanyika kuanzia wiki ya tatu baada ya tamko la kusimamisha ligi," alisema Magori

Lakini pia uamuzi huo huenda ukaviumiza zaidi vilabu ambavyo kwa kiasi kikubwa ukiondoa Simba, Azam na Yanga, vingine vinajiendesha kwa mapato hayo ya milangoni

Post a Comment

0 Comments