BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TAREHE 30-03-2020

Real Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal raia wa Gabon Emerick Aubameyang,30, endapo watashindwa kumpata Erling Braut Haaland, 19, kutoka Borussia Dortmund ama mchezaji wa kimataifa wa Senegal Sadio Mane, 27 kutoka Liverpool. (Express)
Real pia wanataka kumsajili kiungo wa kati Mbrazili wa miaka 21, Igor Gomes, ambaye bei yake huenda ikawa £45m kutoka Sao Paolo.(AS - in Spanish)
Newcastle United wanapania kuwasajili kwa mkopo wachezaji wa safu ya kati ya Robbie Brady na Jeff Hendrick, walio na miaka 28. Mkataba wa wachezaji hao wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland katika uwanja wa Turf Moor unamalizika msimu huu wa joto. (Newcastle Chronicle)
Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan ana matumaini ya uhamisho wake wa mkopo kwenda Roma utageuzwa kuwa mkataba wa kudumu msimu huu . Arsenal wanataka £18m kumuachilia kiungo huyo wa miaka 31- raia wa Armenia, lakini klabu hiyo ya Italia inataka kulipa £10m tu. (Mail)
Erling Braut Haaland ni mchezaji anayeng'ara barani ulaya kwa sasa na kiwango chake hakijawahi kushuka tangu alipojiunga na Borussia DortmundHaki miliki ya pichan
Nyota wa zamani wa Barcelona Uhispania Xavi anasema yuko tayari kuwa mkufunzi wa klabu hiyo ya La Liga lakini anasisitiza hakutakuwa na gumzo la "kuvunja moyo" katika chumba cha kubadilisha nguo. (La Vanguardia - in Spanish)
Kipa wa Aston Villa wa mika 33 , Muingereza Tom Heaton anataka kufanya kazi ya ukufunzi atakapostaafu na angelipendelea kurejea katika klabu yake ya zamani ya Burnley. (Independent)

Everton wana matumaini kuwa ramani ya mapendekezo ya kujenga uwanja mpya itaidhinishwa msimu huu wa joto, licha ya kuwepo kwa janga la coronavirus. (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20, anafaa kuchukua fursa na kujiunga na Manchester United, kulingana na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Dimitar Berbatov. (Sun)
Sadio ManeHaki miliki ya pichan
Chelsea ina hamu ya kumsaini kipa wa Ujerumani Manuel Neuer, 34, ambaye amekuwa katika klabu ya Bayern Munich tangu 2011. (Bild)
Bayern itamtumia mchezaji mwenza wa Neuer , Marc-Andre ter Stegen. Kipa huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 27 huenda akagharimu £90m. (Daily Mail)
Beki wa England John Stones, 25, huenda akaondoka katika klabu ya Manchester City, huku beki wa kati wa Juventus na Italy Leonardo Bonucci, 32, akitarajiwa kuchukua mahala pake. (Star)
Tottenham inataka kumsaini beki wa Intermilan na Uruguay Diego Godin, 34, huku kocha wa Spurs Jose Mourinho akitazamiwa kuimarisha safu yake ya ulinzi . (Mirror)
Everton na West Ham wanafikiria kumsaini mshambuliaji wa Barcelona na Denmark Martin Braithwaite, 28, ijapokuwa klabu yake Barcelona haitamuuza kwa chini ya dau la £16m. Braithwaite alijiunga na Barca mwezi Februari katika usajili wa dharura. (Diario Sport - in Spanish)
Nyota wa zamani wa Barcelona Uhispania Xavi anasema yuko tayari kuwa mkufunzi wa klabu hiyo ya La LigaHaki miliki ya pichan
Arsenal inataka kumsaini kiungo wa kati wa Valencia na uhispania Carlos Soler, 23, ambaye hivi karibuni alitia saini kandarasi mpya hadi 2023.. (Sun)
Janga la coronavirus limeathiri kurudi kwa mchezaji wa Chelsea Ruben Loftus cheek ambaye alikuwa akiugua jeraha la kifundo cha mguu huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akishindwa kujiimarisha. Loftus Cheek hajawahi kucheza tangu mwei 2019 (Evening Standard)

Post a Comment

0 Comments