BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TAREHE 02-03-2020

Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19, hana mawazo kuhusiana na hatma yake ya baadae licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kuenda Manchester United ama Liverpool. (Mail)
Tottenham wanajiandaa kumsaka kipa wa Watford Ben Foster, 36, ambaye mkataba wake Vicarage Road unamalizika msimu huu wa joto. (Sun)
Spurs pia wanataka kuikosesha Roma nafasi ya kumpata Chris Smalling kutoka Manchester United kwani wana mpango wa kumpatia mkataba wa kudumu.
Beki huyo wa England, 30 ,kwa sasa yuko katika klabu hiyo ya Italia kwa mkopo. (Calciomercato, in Italian)
Chris SmallingHaki miliki ya picha
Image captio
United pia wanamfuatilia beki wa Stoke City Nathan Collins, Kiungo huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland aliye na umri wa chini ya miaka 21, amecheza mara 12 katika timu ya kwanza ya Potters. (Sun)
Dries Mertens ,31, anayelengwa na Chelsea anakaribia kusaini mkataba mpya katika klabu ya Napoli. Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Ubelgiji inakamilika msimu huu wa joto. (Sun)
Kalidou KoulibalyHaki miliki ya picha
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta huenda akapewe fedha kidogo ya za kununua wachezaji msimu huu wa joto ikiwa klabu hiyo itashindwa kufuzu kwa Champions League msimu ujao licha ya tetesi kuibuka kuhusu hali ngumu ya kifedha inayokumba klabu hiyo. (Goal)
Afisa mkuu mtendaji wa Inter Milan Giuseppe Marotta anahofia msimu wa ligi kuu ya Italia Serie A huenda usimaliziki ikiwa hawatapata suluhisho janga la kiafya la coronavirus. (Mail).
Cristiano Ronaldo, 35, amesema kwamba anafurahia kuwa Juventus na hana nia ya kujiunga na Inter Miami inayomilikiwa na David Beckham. (Sky Sports)
Barcelona inamnyemelea mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 30 ambaye mkataba wake unamlizika mwisho wa simu ujao. (Sunday Express)
Cristiano RonaldoHaki miliki ya picha
Manchester United wako tayari kutoa kima cha £150,000 kwa wiki kwa nahodha wa Aston Villa Jack Grealish ili kuwa Old Trafford katika msimu ujao wa uhamisho. (Sun)
Mshamambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland ndiye anayependelewa na Real Madrid wakati inapojiandaa kuongeza mshambuliaji mwengine kwa msimu wa tatu mfululizo.
Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, pia yuko kwenye orodha ya Real Madrid na kumaanisha kwamba huenda Liverpool ikapata upinzani wa kumpata mchezaji huyo wa Ujerumani. (Daily Mail)
Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, yuko kwenye orodha ya Real MadridHaki miliki ya picha
Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford ana imani kwamba ataweza kurejea uwanjani kabla ya mwisho wa msimu huu kutokana na jeraha la mgongoni.
Liverpool itakuwa na kibarua cha kuimarisha safu yake ya mashambulizi msimu ujao kwasababu mchezaji wa kimataifa Adam Lallana, 31, na Xherdan Shaqiri, 28, wa Switzerland wote wanatarajiwa kuondoka mwisho mwa msimu. (The Athletic via Express)

Post a Comment

0 Comments