BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATANO TAREHE 25-03-2020


Winga wa Manchester City na England Raheem Sterling, 25, bado ana mapenzi na Liverpool licha ya kuondoka klabuni hapo kwa mazingira ya chuki. (Sky Sports)
Klabu za Liverpool, Manchester City na Arsenal zinavutiwa kumsajili beki kinda wa Schalke Malick Thiaw, 18, na mwenye urefu wa futi 6.3 ambaye mkataba wake umeweka Lima cha mauzo ya usajili cha pauni milioni 6.9. (Mail)
Klabu ya Manchester United inaendelea kuamini kuwa kiungo nyota wa Ufaransa Paul Pogba, 27, ataendelea kusalia Old Trafford huku wakitilia mashaka juu ya uwezo wa klabu yeyote kubwa Ulaya kumnunua. (ESPN)

Klabu ya Manchester United inaendelea kuamini kuwa kiungo nyota wa Ufaransa Paul Pogba, 27 ataendelea kusalia Old TraffordHaki miliki ya pichS

Real Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 19, japo klabu za Manchester United na Tottenham pia zimeonesha nia ya kumsajili. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Chelsea wameweka malengo ya kumsajili beki wa pembeni wa Getafe Marc Cucurella, 21, mwishoni mwa msimu kwa pauni milioni 23. (Diario Sport - in Spanish)
Klabu hiyo pia inavutiwa na beki wa Ajax Nicolas Tagliafico, 27, hususani baada ya kuachana na mipango ya kumsajili beki wa Leicester Ben Chilwell. (Calciomercato via Daily Express)

Beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, ambaye yupo kwa mkopo RomaHaki miliki ya pichaS

Beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, ambaye yupo kwa mkopo Roma anaweza akasajiliwa moja kwa moja na klabu hiyo endapo United watamsajili beki wa Senegal Kalidou Koulibaly kutoka klabu ya Napoli. (Gazzetta dello Sport via Football Italia)
Wachezaji na wafanyakazi wa Juventus leo wanamaliza muda wao wa kujitenga na wataruhusiwa kutoka majumbani mwao.
Hata hivyo wachezaji watatu Daniele Rugani, Blaise Matuidi na Paolo Dybala watasalia karantini wakiendelea na matibabu ya virusi vya corona. (Gazzetta dello Sport)

Post a Comment

0 Comments