BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAPILI TAREHE 22-03-2020


Ligi ya Primia kwa mara nyingine tena inachunguza jinsi ya kucheza micheze ndani ya nyumba wakati huu wa mzozo wa coronavirus ili kukamilisha msimu wa soka . (Independent)
Manchester United wanafanya mazungumzo na kiungo wa kati Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, juu ya mkataba mpya wa miaka miwili wenye thamani ya £140,000-wiki moja baada ya kufanyia marekebisho ya kipengele cha mkataba ili kurefusha zaidi mkataba wa Mserbia huyo kwa mwaka mmoja zaidi. (Sun)

Wilfried Zaha amejitolea kwa mali zake kusaidia katika vita dhidi ya coronavirusHaki miliki ya pichan

Winga wa Crystal Palace kutoka Ivory Coast Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 27, amejitolea kutoa nyumba zake 50 ilizitumiwe na wahudumu wa afya ya umma nchini Uingereza wanaopambana na mlipuko wa coronavirus katika katika hospitali za London. (Times - subscription required)
Mshambuliaji wa West Brom Charlie Austin amewataka watu coronavirus baada yay eye binafsi kupata virusi hivyo. Muingereza huyo mwenye umri wa 30 anashuku alipata virusi vya corona katika tamasha la Cheltenham. (Telegraph - subscription required)

Mshambuliaji wa safu ya kati wa Chelsea Willian anaomba arudi kwao BrazilHakImage caption

Mshambuliaji wa safu ya kati wa Chelsea Willian, mwenye umri wa miaka 31, ameitaka klabu impe ruhusa ya kurudi katika nchi yake ya kuzaliwa-Brazil ili awe na familia yake . (Mirror)
Klabu zinazoongoza katika championi zinaangalia uwezekano wa mpango kupunguza malipo ya mchezaji kwa pauni £6,000 kwa wiki kwasababu ya kuahirishwa kwa msimu wa soka. (Telegraph - subscription required)
Winga wa Sassuolo Jeremie Boga, mwenye umri wa miaka 23, anaweza kurejea Chelsea kwasababu the Blues wanakipengele cha kumnunua tena kwa pauni milioni £12. Katika mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast.(Mail)

Winga wa Sassuolo Jeremie Boga anaweza kurejea ChelseaHaki miliki ya picha

Juventus wanataka kuwapatia Chelsea kiungo wa kati Mbosnia-Herzegovina Miralem Pjanic, mwwenye umri wa miaka 29, kama sehemu ya mkataba wa kubadilishana wachezaji Juventus wakimtaka kiungo wa kati Mtaliano Jorginho mwenye umri wa miaka 28 . (Corriere dello Sport, via Su

Mshambulia Odion Ighalo amekua akipokea marupurupu makubwa katika Old TraffordHaki miliki ya pichan

Mchezaji anayeichezea Manchester United kwa deni katika safu yao ya mashambulizi Odion Ighalo, mwenye umri wa miaka 30, analipwa pauni £8,000 kwa kila goli analolifunga na pauni £9,000 kwa kila ushindi juu ya mshahara wake wa juu wa pauni £180,000-anazolipwa kila wiki katika Old Trafford. (Sun)
Mbrazil anayecheza safu ya ulinzi katika blabu ya Lille nchini Ufaransa Gabriel Magalhaes,mwenye umri wa miaka 22, yuko katika orodha ya Everton uhamnisho ya msimu.(Liverpool Echo)

Barcelona na Real Madrid wanaweza kumnunua difenda wa Austria mwenye umri wa miaka 27- David Alaba,Haki miliki ya pichan

Mlindalango wa Italy Gianluigi Donnarumma, mwneye umri wa miaka 21, ataondoka AC Milan na kuhamia katka klanu ya Ufaransa ya Paris St-Germain au Primia Ligi. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Barcelona na Real Madrid wanaweza kumnunua difenda wa Austria mwenye umri wa miaka 27- David Alaba, ambaye hana uhakika juu ya kuongezewa kwa mkataba katika klabu Bayern Munich.(Bild - in German)

Atletico Madrid inaangalia uwezekano wa kuendelea kuwa na Mghana Thomas Partey kikosini huku timu maarufu za England zikimtakaHaki miliki ya t

Liverpool wamekua na mazungumzo "kwa muda " na kiungo wa kati wa timu ya Ufaransa Lille ya wachezaji wenye chini ya umri wa miaka 21 Boubakary Soumare. (Sport - in Spanish)

Post a Comment

0 Comments