Uefa inafikiria kuahirisha mashindano ya Euro 2020 hadi Desemba ili kuwa na muda wa kutosha kwa Ligi ya Premier na mashindano mengine ya vilabu kumalizika baada ya kutokea kwa janga la Corona. (Sunday Telegraph)
Mshambuliaji wa Manchester City Riyad Mahrez, 29, ana mpango wa kuhamia Paris St-Germain, ambayo imeonesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa Algeria msimu ujao. (Calciomercato via Express)
PSG inatarajia mshambuliaji wao wa Brazil Neymar, 28, kuhama Klabu hiyo msimu ujao na kurejea katika iliyokuwa klabu yake ya zamani Barcelona kwa kitita cha euro milioni 150. (Marca - in Spanish)
Barcelona inakaribia kuachana na dhamira yao ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (Sunday Express)
Real Madrid imelenga zaidi mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, 27, dirisha la usajili litakapofunguliwa (Mirror)
Chelsea iko mbioni kutafuta euro milioni 85 kwa winga wa klabu ya Bayer Leverkusen na Jamaica Leon Bailey, 22, baada ya kupendezwa na mchezo wake alipokuwa akichezea Bundesliga katika ligi ya Ulaya. (Sunday Express)
Chelsea imeingia kwenye kinyang'anyiro kati yake na Napoli, Borussia Monchengladbach na Bayer Leverkusen cha kutaka kumsajili mchezaji wa Barcelona, Marc Cucurella, 21, ambaye anachezea Getafe kwa mkopo na timu zote hizo zimeonesha nia ya kutaka kumsajili mlinzi huyo wa Uhispania. (Mail on Sunday)
Kiungo wa kati wa Valencia Geoffrey Kondogbia, 27, analengwa na Tottenham, ambaye amemvutia kocha wa Spurs Jose Mourinho. (Goal)
Mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez, 28, yuko tayari kuondoka Wolves akiwa na uwezekano mkubwa wa kusajiliwa na Manchester United lakini klabu yake itakubali hilo kwa ofa ya juu tuu wala si vyenginevyo. (Manchester Evening News)
Juventus inatafuta kiungo wa kati na wameelekeza macho yao kwa raia wa Italia, 19, Sandro Tonali wa Brescia na mfaransa, 21, Houssem Aouar wa Lyon wakati ambapo matumaini ya kumrejesha Paul Pogba, 27, katika klabu hio kutoka Manchester United yakianza kudidimia. (Tuttosport - in Italian
Newcastle United inatafuta kumsajili mlinzi wa Manchester United na Uingereza Phil Jones, 28. (Sunday Mirror)
Mlinda lango wa Ajax na Cameroon Andre Onana, 23, anagunwa gunwa kutaka kuhamia Chelsea baada ya mchezaji wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, kuwekwa benchi kwa matokeo mabaya. (Sunday Express)
Mshambuliaji Emerson Palmieri anawindwa na Juventus, ikiwa tayari kutoa ofa ya £25m kwa Chelsea na mchezaji huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 25. (Sun on Sunday)
Na huku michuano ya ligi ya Premier ikiwa imeahirishwa, wachezaji wa Liverpool, wafanyakazi na mashabiki wamejumuika na timu hiyo kuchangisha pesa za kununua chakula cha akiba ambayo inategemea msaada kutoka kwa wafadhili. (Liverpool FC)
0 Comments