BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAPILI TAREHE 1 MACHI 2020

Mlinda lango wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, anamejitayarisha kuondoka Chelsea msimu huu baada ya kukosa nafasi kwenye timu. (Sun)
Arrizabalaga yuko tayari kuondoka Stamford Bridge kwasababu maneja Frank Lampard alishindwa kutimiza makubaliano yao ya mdomo kwamba ampe kipaumbele. (Mail)
Hata hivyo, Lampard anasema Arrizabalaga ndiye anayedhibiti hatma yake mwenyewe katika klabu hiyo. (Sky Sports)
Maneja wa Leicester Brendan Rodgers anasema jeraha kwa mshambuliaji Jamie Vardy i tatizo baada ya mchezaji huyo, 33, kukosa mechi waliocharazwa na Norwich baada ya kuumia mguuni. (Leicester Mercury)
Maneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ametuma watu wake kumtazama mchezaji winga wa kimataifa wa Italia Federico Chiesa, 22, ambaye huenda akawagharimu £60m. (Mail)
Mesut Ozil prays before Arsenal's game against Manchester CityHaki miliki ya picha
Kiungo Merumani wa Arsenal Mesut Ozil, 31, amethibitisha kwamba kamwe hataondoka Arsenal kabla ya mkataba wake kumalizika Juni 2021. (inews)
Kiungo wa kati wa Aston Villa, Jack Grealish, 24,ameonyesha kwamba anapanga kusalia katika klabu yake msimu huu licha ya kwamba Manchester United imeonyesha nia ya kumuhitaji. (Express)
Lakini maneja wa Villa Dean Smith hana uhakika ikiwa Grealish atasalia katika klabu hiyo bila kutilia maanani iwapo klabu hiyo itashinda kombe la ligi dhidi ya Manchester City Jumapili au la. (Mirror)
Aliyekuwa kocha wa Villa Alex McLeish ametoa siri kwamba nusura Manchester United imsaini Grealish kwa kima cha £200,000 peke yake mwaka 2012. (Mail)
Kiungo wa kati wa Everton kutoka Ureno Andre Gomes, 26, anasema alikuwa na malumbano na kocha msaidizi Luis Boa Morte punde tu baada ya kupata jeraha baya la kifundo cha mguu November. (Star)
Emil ForsbergHaki miliki ya picha
Kiungo wa RB Leipzig, 28, Emil Forsberg anasema kwamba sio jambo la kushangaza kuwa kocha wa Tottenham Jose Mourinho angependa kuwa naye katika timu yake. (Expressen - in Swedish)
Leicester City inakaribi akumsajili kmchezaji kijana wa Ufaransa Arnaud Lusamba, 23, bila malipo punde tu mkataba wake wa Nice ukapomakamilika mwishoni mwa msimu huu. (Mail)
West Ham itamruhusu mchezaji Nathan Holland, 21, kuondoka kwa kima cha £2m pekee msimu huu. (Football Insider)
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kwamba ilikuwa vizuri baada ya mchezaji wa RB Leipzig na mshambuliaji wa Ujerumani Tim Werner kusema kwamba anafurahia kuhusishwa na kuhamia Liverpool. (Sky Sports)
Hakuna uhakika kwamba mabigwa wa ligi ya Premier wataibuka na ubingwa katika ligi ya Uingereza msimu huu iwapo mechi zilizopagwa zitakatishwa kwa hofu ya coronavirus. (Telegraph)
Na ligi ya Premier itafanya mazungumzo ya dharura kuamua ikiwa Liverpool itatangazwa kuibuka na ushindi iwapo msimu huu utasimamishwa mapema kwa hofu ya coronavirus. (Sun

Post a Comment

0 Comments