Manchester City itazuia uhamisho wa winga wa Algeria Riyad Mahrez, 29, wa kujiunga na Paris St-Germain msimu wa joto. (Goal)
Manchester United inapania ku saini mkataba na beki wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti, 26, msimu huu. (Sport - in Spanish)
Chelsea imeipatia kipaumbele mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Moussa Dembele, 23, dirisha la usajili wa wachezaji litakapofunguliwa msimu wa joto. (The Athletic - subscription required)
Blues wameripotiwa kuwasiliana na Porto kuhusu uhamisho wa wa beki wa Brazil Alex Telles, 27. (A Bola, via Sun)
Chelsea na Manchester City wanamfuatilia mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez. Nyota huyo wa miaka 22 pia ananyatiwa na Barcelona. (Sport - in Spanish)
Beki wa Liverpool na Croatia Dejan Lovren, 30, anang'ang'aniwa na Arsenal na Tottenham. (Mirror)
Beki England Leighton Baines, 35, anataka kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na Everton licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kuenda LA Galaxy. (The Athletic - subscription required)
Jurgen Klopp anapanga kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake cha Liverpool ambayo huenda yakajumuisha wachezaji sita kuondoka klabu hiyo. (Mirror)
Beki wa Manchester United Mreno Diogo Dalot, 20, anasema mchezaji mwenzake Bruno Fernandes atakuwa "shujaa" wa klabu hiyo. (Sky Sports)
Everton wanajiandaa kuungana na Inter Milan kumsaka kiungo wa kati wa Roma na Italia Lorenzo Pellegrini, 23. (Calciomercato - in Italian)
0 Comments