BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAMOSI TAREHE 28-03-2020

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20, anafaa kuchukua fursa na kujiunga na Manchester United, kulingana na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Dimitar Berbatov. (Sun)
Chelsea ina hamu ya kumsaini kipa wa Ujerumani Manuel Neuer, 34, ambaye amekuwa katika klabu ya Bayern Munich tangu 2011. (Bild)
Bayern itamtumia mchezaji mwenza wa Neuer , Marc-Andre ter Stegen. Kipa huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 27 huenda akagharimu £90m. (Daily Mail)
Marc-Andre ter StegenHaki miliki ya picha
Beki wa England John Stones, 25, huenda akaondoka katika klabu ya Manchester City, huku beki wa kati wa Juventus na Italy Leonardo Bonucci, 32, akitarajiwa kuchukua mahala pake. (Star)
Tottenham inataka kumsaini beki wa Intermilan na Uruguay Diego Godin, 34, huku kocha wa Spurs Jose Mourinho akitazamiwa kuimarisha safu yake ya ulinzi . (Mirror)
Beki matata wa Atletico Madrid Diego GodinHaki miliki ya pichao
Everton na West Ham wanafikiria kumsaini mshambuliaji wa Barcelona na Denmark Martin Braithwaite, 28, ijapokuwa klabu yake Barcelona haitamuuza kwa chini ya dau la £16m. Braithwaite alijiunga na Barca mwezi Februari katika usajili wa dharura. (Diario Sport - in Spanish)
Arsenal inataka kumsaini kiungo wa kati wa Valencia na uhispania Carlos Soler, 23, ambaye hivi karibuni alitia saini kandarasi mpya hadi 2023.. (Sun)

Post a Comment

0 Comments