BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAMOSI TAREHE 14-03-2020

Liverpool bado ina uwezekano mkubwa wa kutwaa taji la ligi ya Premier hata wakati ambapo coronavirus imesababisha msimu kuhairishwa. (Telegraph)
Naibu mwenyekiti wa West Ham United Karren Brady amesema kuwa msimu wa ligi ya Premier unastahili kufutiliwa mbali kabisa ikiwa hakuna mechi zingine zitakazochezwa. (Sun)
Kocha wa Leeds United Marcelo Bielsa TEMP ameamua kwamba kikosi chake kitakuwa kinafanya mazoezi katika wakatiambapo msimu wa ligi ya Premier umeahirishwa kwasababu ya virusi vya Corona. (Mail).
Vilabu vingi vimekumbwa na changamoto katika hatua yao ya kufuatilia kwa karibu wachezaji ambao huenda wangetaka kuwasajili kwasababu ya marufuku ya usafiri, mechi kuchezwa katika maeneo yasiyoruhusiwa watu na kuhairishwa ligi. (Independent)
Ligi ya Champions huenda likakamilika na robo fainali huku nusu fainali ikichezwa katika ligi nyingine. (Mirror)
Vilabu vinavyoshiriki ligi ya Premier huenda vikataka kucheza msimu utakapoanza tena Aprili kwa sababu ya wasiwasi wa hali ya wachezaji wao na uadilifu wa mashindano hayo. (Mail)
West Ham na Tottenham Hotspur zina shinikizo la kumaliza michezo yao ya nyumbani huku michezo mingi ya msimu wa joto ikiwa tayari imeshapangiwa kuchezwa katika viwanja vyao. (Mirror)

Diogo JotaHaki miliki ya pichan

Arsenal sasa inafikiria uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Wolves Diogo Jota, 23. (Mail)
Juventus imemlenga Houssem Aouar, 21, kama kiungo wa kati mbadala iwapo itamkosa mchezaji wa kiamtaifa wa Manchester United Paul Pogba, 26.(Calciomercato - in Italian)
Chelsea inafuatilia kwa karibu kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Angel Gomes, 19, katika uhamisho wa bila malipo. (Metro)

Denis ZakariaHaki miliki ya pichao

Manchester United wako kifua mbele katika kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji wa Borussia Monchengladbach, kiungo wa kati wa Switzerland Denis Zakaria, 23, ambaye pia anawindwa na Liverpool, Atletico Madrid na Borussia Dortmund.(Sky Germany, via Mirror)
Barcelona imekubali kumsaini mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez kutoka Inter Milan msimu ujao wa usajili na mchezaji huyo, 22, atapewa kandarasi ya mwaka mmoja kwa kitita cha £16m. (Star)
Juventus itatoa ofa ya £25m kwa mshambuliaji wa Chelsea raia wa italia Emerson Palmieri msimu ujao baada ya ombi lao kukataliwa January. (Express)
Lazio anataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea raia wa Ufaransa, Olivier Giroud, 33, na kiungo wa kati wa AC Milan raia wa Italia, Giacomo Bonaventura, 30, baada ya kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Mathis Rayan CherkiHaki miliki ya picha

Barcelona na Real Madrid zote zinamwinda mshambuliaji wa Lyon, 16, Rayan Cherki. (Calciomercato - in Italian)
Maneja wa Burnley Sean Dyche anasema ni jambo lisiloweza kuepukika kwamba siku moja lazima The Clarets haitakuwa na budi zaidi yakumuachilia winga Dwight McNeil lakini kwa sasa hawana haraka hiyo ya kumuuza mchezaji huyo wa miaka 20. (Mirror)

Post a Comment

0 Comments