BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMISI TAREHE 19-03-2020

Arsenal wanasaini upya mkataba wa kumpoteza mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa miaka 30, msimu huu na wanataka garama ya euro milioni 55 (£50.7m) kwa ajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon ambaye anatafutwa Barcelona. (Sport, in Spanish)
Borussia Dortmund wamesonga mbele ya Liverpool, Manchester United na Chelsea katika kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na kiungo wa kati wa kikosi cha England cha vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Jude Bellingham, mwenye umri wa miaka 16, kutoka Birmingham msimu huu. (Bild, in German)
Manchester City, Juventus na Paris St-Germain wameonyesha nia ya kusaini mkataba na kiungo wa kati Mfaransa Houssem Aouar, mwenye umri wa miaka 21, kutoka klabu ya Ufaransa ya Lyon. (Corriere dello Sport, in Italian)
Jude Bellingham anasakwa na timu tatu za EnglandHaki miliki ya pichan
Arsenal wamefanya mazungumzo na Hammarby juu ya kusainiwa kwa mkataba na mchezaji kutoka kikosi cha kimataifa cha vijana wadogo cha Sweden Emil Roback, mwenye umri wa miaka 16, anayecheza skatika safu ya kati ya mashambulizi ambaye pia Bayern Munich wameonyesha azma ya kutaka kumnunua. (Daily Mail)
Arsenal pia watafanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Villarreal Santi Cazorla katika msimu huu ili kumpatia fursa ya kusema kwaheri kwa mashabiki wake. Muhispania huyo mwenye umri wa miaka 35-aliondoka Gunners katika msimu wa majira ya joto wa mwaka 2018,baada ya kutocheza mechi kwa karibu miaka miwili kwasababu ya jeraha alilokuanalo. (Daily Express)
Manchester City, Juventus na Paris St-Germain wote wameonyesha nia ya kusaini mkataba na kiungo wa kati Mfaransa Houssem AouarHaki miliki ya pichaa
West Ham wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya kimchezo ya difenda Muingereza Dion Sanderson, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika Cardiff kutoka Wolves. (Daily Mail)
Chelsea wamezungumza na Barcelona kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba na kiungo wa kati Mbrazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 27, kwa mkopo msimu ujao. (Sport, in Spanish)
Manchester City na Manchester United wako tayari kumchukua kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, huku kijana huyo mwanye umri wa miaka 25- akihangaika kusaini mkataba mpya na Atletico Madrid. (Mundo Deportivo, in Spanish)
Mbrazil Philippe Coutinho huenda akachukuliwa na BarcelonaHaki miliki ya pichan
Inter Milan wako tayari kumpa mkataba wa mwaka mmoja zaidi Muingereza Ashley Young, mwenye umri wa miaka 34, baada ya kuwafurahisha kimchezo tangu alipohamia kikosini mwezi Januari kutoka Manchester United. (Gazzetta dello Sport, in Italian)
Shirikisho la soka la Ireland linamtaka meneja wa Stoke Michael O'Neill kuendelea kuongoza mechi za timu ya taifa ya Ireland Kaskazini kwa ajili ya Euro 2020, ambazo zimeahirishwa hadi Juni kwasababu ya janga la coronavirus. (Daily Mirror)
Mjamaica Leon Bailey anafuatiliwa na Arsenal na Chealsea
Dau la Aston Villa kwa ajili ya kiungo wa kati wa Angers Baptiste Santamaria lilikataliwa mwezi Januari na bado hawajaamua ikiwa watatoa pesa zaidi kwa ajili ya kijana huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 25-msimu huu. (ABC Sevilla, in Spanish)
Arsenal na Chelsea wote wanamfuatilia kwa karibu maendeleo ya kimchezo ya mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Mjamaica Leon Bailey, mwenye umri wa miaka 22 ambaye amethamanishwa kwa kiwango cha pauni milioni 85 . (Daily Express)
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anataka kumuuza kiungo wa kati wa Armenia Henrikh MkhitaryanHaki miliki ya picha
Beki wa Atletico Madrid na Kieran Trippier, 29, amedokeza kuwa atastaafu katika klabu yake ya zamani Burnley na kwamba atarejea katika ligi ya Primia ikiwa atacheza Turf Moor chini ya Sean Dyche. (Sky Sports)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anataka kumuuza kiungo wa kati wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 31, msimu wa joto huku wakiwa na mpango wa kubadili mkataba ake wa mkopo kuwa uhamisho wa kudumu . (Express)

Post a Comment

0 Comments