BETI NASI UTAJIRIKE

TATHMINI: LIVERPOOL YAPIGWA ANFIELD, DORTMUND YATUPWA NJE UEFA




Usiku wa jana ulikuwa mgumu kwa mashabiki wa Liverpool na Borrusia Dortmund baada ya timu hizo kuondoshwa hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya. Liverpool wakiwa nyumbani walishindwa kutamba mbele ya vijana wa Diego Simeone.

Uchambuzi wa Mechi

Paris Saint Germain vs Borrusia Dortmund 

Borrusia Dortmund walikuwa na nafasi kubwa kuweza kufuzu hatua ya robo fainali baada ya mchezo wa kwanza kushinda 2-1 wakiwa nyumbani na walitakiwa watafute sare yoyote dhidi ya PSG . Mambo yalikuwa mazuri kwa PSG wakiwa nyumbani Le Parc des Prince baada ya kushinda mabao 2-0 kupitia kwa Neymar Jr aliyefunga bao dakika ya 28 huku Juan Vlasco akishindilia ushindi kwa bao la dakika 45 z kipindi cha kwanza. 

PSG walicheza vizuri eneo la kiungo na kufanikiwa kuzima kabisa mipango ya Dortmund. Uwepo wa Neymar Jr ,Cavani na Di Maria uliongeza utamu wa mchezo huo.

Kwa mtokeo hayo PSG anasonga mbele kwa wastani wa mabao 3-2 




Liverpool Vs Atletico Madrid

Vijana wa Diego Simeone walionyesha weredi wa hali ya juu kwenye eneo la ulinzi na kuzuia utatu mtakatifu wa Mane Salah na Firmino kufanya yao. Kichwa cha Wijnaldim dakika ya 43 kiliibua shangwe Anfield na mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Liverpool walikuwa mbele kwa bao 1-0 huku wakilisakama lango la Atletico Madrid ambao walizuia kwa dakika zote 90.

Mpaka dakika 90 zinamalizika Liverpool walikuwa mbele kwa bao 1-0 na refa alilazimika kuongeza dakika 30 zilizogeuka chungu kwa Liverpool. Dakika ya 95 Firmino aliiandikia liverpool bao la kuongoza lakini Super Sub Marcos Llorente aliyeingia kuchukua nafasi ya Diego Costa alilijibu bao hilo dakika ya 97 na 105 akapachika jingine na kufanya matokeo kuwa 2-2 kwa dakika 105.

Dakika 106- 120 Liverpool walikuwa mwiba mkabili kwenye eneo la Atletico wakiwa na lengo la kurudisha mabao hayo lakini super sub Morata aliyechukua nafasi ya Joao Alex aligeuka  mwiba na kufunga bao la tatu na kuifanya Liverpool iodoshwe kwa jumla ya mabao 4-2



Post a Comment

0 Comments