BETI NASI UTAJIRIKE

TARIQ SEIF AFUNGUKA KILICHOPELEKEA SARE NA NAMUNGO FC
Mshambuliaji wa Yanga Tariq Seif amesema kuwa walitengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuibuka na ushindi mbele ya Namungo FC kutokana na kukosa umakini.

Yanga wakati ikikubali kutoshana nguvu na Namungo FC Uwanja wa Majaliwa kwa kufungana bao 1-1 wao walianza kufunga bao dk ya sita kupitia kwa Seif kabla ya Namungo kuweka mzani sawa dk ya 62 kupitia kwa Bigirimana Blaise.

Nyota huyo amesema: "Tulitengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo na kushindwa kuzitumia kutokana na kukosa umakini ndani ya uwanja, tutafanyia kazi mapungufu yetu,".

Mchezo uliopita Yanga ilipoteza pointi tatu mazima mbele ya KMC jana Machi 15 imegawana pointi mojamoja na Namungo FC kwenye mchezo wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara.

Bao hilo la kichwa alilofunga Seif ni la tatu ndani ya ligi ambapo la kwanza aliwafunga Biashara United kwa pasi ya Papy Tshishimbi akafunga mbele ya Polisi Tanzania kwa pasi ya Bernard Morrison na jana alifunga kwa pasi ya Juma Abdul.

Post a Comment

0 Comments