BETI NASI UTAJIRIKE

TAMBWE MAGOLI KUTUA DAR KISA SIMBA NA YANGA ,ATAJA TIMU ATAKAYOSHANGILIA


Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Simba Amissi Tambwe amesema atakuja nchini March 07  kushuhudia mchezo wa pili wa watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Taifa Jumapili, March 08
Tambwe alijiunga na Fanja Fc ya Oman baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika lakini ameondoka hivi karibuni kwa kile alichoeleza kurudi kwao Burundi kushughulikia matatizo ya kifamilia
Kuelekea mchezo huo, Tambwe amesema ana imani kuwa Yanga itafanya vizuri zaidi ya mchezo wa kwanza ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2
Mshambuliaji huyo anayeshikilia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote kwa ligi kuu ya Tanzania kwa wachezaji wa kigeni, amesema Yanga imeimarika ukilinganisha na wakati ilipokuwa ikinolewa na kocha Mwinyi Zahera
"Nakuja Tanzania, Jumapili naweza kuja uwanjani kuangalia mchezo. Hautakuwa mwepesi kwa kila timu kwani hata Yanga ninavyoiona sasa imeimarika kuliko ilivyokuwa mwanzo," alisema
"Timu inaonekana kuwa na mabadiliko makubwa, inacheza vizuri labda shida kidogo wanayo kwenye safu ya ushambuliaji. Lakini naamini kwenye mchezo huo watajitolea kwa nguvu zote hivyo lolote linaweza kutokea"
"Unajua hii michezo ya Simba na Yanga wakati mwingine matokeo huwa vile isivyotarajiwa. Mfano ni mchezo wa kwanza waliocheza mwaka huu, Simba walikuwa na uhakika kuwa wangeshinda lakini haikuwa hivyo"
"Hivyo huwezi kusema ni timu gani itaondoka na ushindi, baada ya dakika 90 kila kitu kitafahamika..."

Post a Comment

0 Comments