BETI NASI UTAJIRIKE

SVEN ATOA SABABU ZA KUTOWATUMIA MARA KWA MARA AKINA AJIB,KICHUYA,NDEMLA,MLIPILI
 Kocha Mkuu wa Simba Sven Van dabroek amesema kuwa wachezaji wake wote ni wazuri ila anashindwa kuwatumia kutokana na kushindwa kumshawishi pale wanapopata nafasi.
Miongoni mwa nyota ambao wamekuwa wakikosekana uwanjani ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya, Said Ndemla, Yusup Mlipili,Beno Kakolanya.
Kichuya, Kakolanya na Ajibu mchezo wao wa mwisho ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Stand United huku Mlipili akiwa nje kwa muda mrefu.
Sven amesema kuwa wachezaji ambao hawatumii bado hawajamshawishi jambo ambalo linamfanya asiwatumie na kutaka wakipata nafasi wafanye kazi kubwa kumshawishi ili wapate nafasi.

"Kuna wachezaji wengi na wote ni wazuri hivyo kinachonifanya nisiwatumie wachezaji wengine ni kushindwa kwao kunishawishi, wakipata nafasi wanatakiwa kuonyeshauwezo wao wote," amesema

Post a Comment

0 Comments