BETI NASI UTAJIRIKE

SIMULIZI: MEDDIE KAGERE ANAVYOWAHARIBIA MABEKI NGULI WA LIGI KUU MSIMU HUU


mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere mwenye mabao 19 ndani ya Ligi Kuu Bara amekuwa na hatari ndani ya kipindi cha pili kuliko cha kwanza kwa kutupia akiwa uwanjani.
Simba ikiwa imecheza mechi 28 kwenye Ligi Kuu Bara inaongoza ikiwa na pointi 71, imefunga mabao 63 huku Kagere akihusika kwenye mabao 24 akifunga 19 na kutoa pasi tano za mabao.
Mabao yake mengi rekodi zinaonyesha amefunga kipindi cha pili ambapo amefunga 10 huku kipindi cha kwanza akifunga mabao 9, bao lake la usiku kwenye ligi ni lile alilofunga dk ya 88 mbele ya Namungo wakati Simba ikishinda mabao 3-2.
Kipindi cha pili amefunga mabao 10 mbele ya JKT Tanzania 1-3 Simba, dk 58,  Kagera Sugar 0-3 Simba dk 79, Simba 1-0 Azam dk 48, Simba 4-0 Lipuli dk 49, Alliance 1-4 Simba dk 58Simba 3-2 Namungo, dk ya 88, Simba 1-0 Kagera Sugar, dk 61, Biashara United wakati Simba ikishinda 3-1 dk 68,  Singida United  dk 70, Azam 2-3 Simba, dk 71.
Kipindi cha kwanza amefunga mabao 9  mbele ya JKT Tanzania 1-3 Simba, dk 1,Simba 2-1
 Mtibwa Sugar dk 17,Kagera Sugar 0-3 Simba dk 4, Simba 4-0, Biashara United 0-2 Simba,
 dk 22, Mbeya City dk 7,Simba 2-2 Yanga dk 42, Simba 8-0 Singida United dk 1 dk 25 dk 41.

Post a Comment

0 Comments