BETI NASI UTAJIRIKE

KAGERE,AJIBU WAZUNGUMZIA MCHEZO WA YANGA , CEO ATANGAZA KUMWAGA PESA


Simba wameipania kwelikweli mechi dhidi ya Yanga Jumapili na wamepanga kufanya kufuru ya aina yake ambayo huenda ikawalaza Yanga na viatu.

Yaani uongozi umeapizana kwamba wanataka kuona mchezo wa kiwango cha juu sana na ikiwezekana idadi kubwa ya mabao kadri inavyowezekana. Mkwanja waliopanga kuwamwagia wachezaji kwenye mechi hiyo ni zaidi ya Sh80mil ambayo ni zaidi ya zawadi ya bingwa wa msimu.

Habari zinasema kwamba Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Simba, Bilionea kijana Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ amepelekewa mapendekezo na Ofisa Mtendaji mkuu, Senzo Mazingisa akayacheki wee..akasema freshi.

Sasa kinachofanyika ni kwamba baadhi ya wajumbe wa Bodi watakwenda kuonana na wachezaji hao kambini kwao, Mbweni watapata chakula cha pamoja siku moja kabla ya mchezo huo na kuwatangazia ahadi hiyo ya kufuru.

Unaambiwa hata yule mchezaji atakayekuwa jukwaani siku hiyo akishangilia na wenzake ataondoka na posho ya Sh1mil ambayo ni mkwanja mnene kuliko mshahara wa staa yoyote wa Mbao mwisho wa mwezi

Habari za ndani zinasema kwamba kila mchezaji atakayecheza hata sekunde moja atapata Sh 4 milioni.Wachezaji ambao watakuwa katika benchi la ufundi ila hawatatumika katika mchezo huo kila mmoja atapata Sh 2mil, wakati wale ambao watakuwa jukwaani kwa maana hawatakuwa katika orodha ya wachezaji 18, kila mmoja atapata Sh 1mil.

Kikosi cha Simba kwa sasa kina orodha ya wachezaji 27, ambao kati ya hao 18, ndio watakuwa katika orodha ya kutumika dhidi ya Yanga kwa maana hiyo wachezaji 11, watakaoanza katika kikosi cha kwanza kama watashinda kila mmoja ataondoka na Sh 4 mil ambayo jumla yake itakuwa Sh 44 milioni.

Benchi la ufundi la Simba kama litafanya mabadiliko ya wachezaji wote watatu kila mmoja atapata Sh 4 mil ambayo kwa ujumla wote watakuwa wamevuta posho ya Sh 7mil kama watashinda.
Wakati wale wanne ambao watabaki katika benchi kwa maana hawatatumika kila mmoja atavuta Sh 2 mil ambayo kwa ujumla wake nao watachukua Sh 8mil. Wakati wale tisa ambao hawatatumika kabisa ambao watakuwa jukwaani kila mmoja atachukua Sh 1mil na jumla yao itakuwa Sh 9 mil.
Kwa maana hiyo motisha ya posho hiyo mgao unaonesha wachezaji pekee yao watachukua Sh 73mil wakati ile nyingine iliyobaki ambayo inaweza kuongezwa kutokana na mikataba yao ilivyo itakwenda kwa benchi la ufundi ambalo lipo chini ya kocha Mbelgiji Sven Vandernbroeck.
Senzo ambaye ni raia wa Sauzi, alisema kutokana na uzoefu aliokuwa nao kwenye mechi yoyote ya watani lazima kunakuwa na mabadiliko ya maandalizi tofauti na michezo mingine lakini hakuweka wazi ni kiasi gani wamewatengea mastaa wao Jumapili.

"Katika mechi zote huwa tunawekaga posho kama tukishinda wachezaji wetu huwa wanapata lakini katika mechi hii ya Yanga tumeziboresha na kuwa kubwa zaidi ya zile za michezo mingine ya kawaida na tumefanya hivi ili kuongeza morali kwa wachezaji wetu na kufikia malengo ya kupata ushindi katika mechi hiyo ya watani ambayo kwetu itakuwa muhimu na kuturahisishia safari yetu ya ubingwa msimu huu," alisema Senzo.

Wachezaji wawili wa Simba, Ibrahim Ajibu na Meddie Kagere kila mmoja alieleza kwa nafasi yake kuwa posho ambayo wanawekewa na viongozi wao katika kila mechi inaongeza morali kwa wachezaji kwanza wenyewe kwa wenyewe kushindana lakini kuweza kujituma na kupata matokeo mazuri.
"Kila mmoja anaonekana kuwa na ari kubwa kuona anapata nafasi ya kucheza na kuitumikia timu ili kufikia malengo yake ya kuondoka na pointi tatu,"
 alisema Kagere.
"Kwa maisha yetu ya kila siku hizi posho ni nyingi kwa hiyo lengo la kwanza ni kujituma kadri ambavyo tunaweza ili kupata ushindi kwani tunatambua kwa upande wetu huu ni mchezo mgumu ndio maana hata motisha kutoka kwa uongozi na maandalizi kwetu yameboleshwa," alisema Ajibu.

Wachezaji hao 27 wa Simba ni Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Pascal Wawa,Tairone Santos, Jonas Mkude, Deo Kanda, Mzamiru Yassin, Kagere, Cletous Chama na Francis Kahata, Hassan Dilunga John Bocco na Benno Kakolanya.
Wachezaji wengine Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Kennedy Juma na Ajibu, Ally Salim, Miraji Athumani, Yusuph Mlipili, Rashid Juma, Sharaf Eldin Shiboub, Haruna Shamte, Rashid Juma, Said Ndemla na Gerson Fraga.

Post a Comment

0 Comments