BETI NASI UTAJIRIKE

MSIMU HUU SIMBA NI NAMBA MOJA KILA SEKTA LIGI KUU



Safu ya ulinzi ya mabingwa watetezi Simba, ndio inang’ara kuliko zote Ligi Kuu Bara, baada ya kufungwa idadi chache ya mabao, huku washambuliaji wao wakiwa tishio kwa kutupia.]

Simba yenye mabeki, Erasto Nyoni, Muivory Coast Pascal Wawa, Kennedy Juma, Mbrazil Tairone Da Silva na Yusuf Mlipili wamekuwa bora baada ya kufungwa mabao 15 tu katika mechi 28 walizocheza mpaka sasa, huku Singida United ikitia fora kwa kuruhusu mabao mengi ambayo ni 48.

Tofauti ya mabao ya Simba inayoonga ligi na Singida United iliyo ya mwisho ni 33
Safu ya mabeki wa Yanga yenye Mghana Lamine Moro, Kelvin Yondani, Juma Makapu, Ally Mtoni na Andrew Vincent ‘Dante’ inashika nafasi ya pili kwa ubora, imefungwa mabao 19, sawa na Coastal Union iliyo nafasi ya tano.

Simba wamekuwa vinara wa kutupia mabao wakiwa wamefunga 63. Mnyarwanda Meddie Kagere, Mkongo Deo Kanda na John Bocco ndio wanaingarisha safu hiyo na Azam FC wa pili, baada ya kufunga mabao 37.

Singida United inaendelea kushikia mkia, licha ya kucheza mechi 28, wamefunga mabao 14 tu. Tofauti kati ya mabao ya Simba na Singida United ni 49, idadi ambao ni kubwa.

Mbali na Simba washambuliaji wa Azam FC wameifanya timu hiyo kuwa wa pili kwa kufunga mabao mengi ambayo ni 37, huku Lipuli FC na Tanzania Prisons wakifuata kwa ubora. Wanashika nafasi ya tatu kila moja ikifunga mabao 35.

Kocha wa JKT, Abdallah Mohammed ‘Bares’ amesema sababu ya Simba kufunga mabao mengi na kufungwa machache ni kutokana na ubora wa safu ya timu yao:

"Wana washambuliaji wazuri wapambanaji ndio maana wamefunga mabao mengi, wana mabeki wazuri ndio maana wamefungwa machache, nawapongeza kwa hilo."
Mlinzi wa Simba Paschal Wawa alisema; "

Sababu kubwa ni ushirikiano uliopo baina yetu mabeki na timu nzima kwa jumla. Kila tunachokifanya tunashirikiana tukiwa na lengo moja ndio maana tumefika hapa."

Post a Comment

0 Comments