BETI NASI UTAJIRIKE

RIPOTI ZA MECHI: MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI LIGI KUU TANZANIA BARA


 Kagera Sugar imekubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Mbeya City FC jioni ya leo uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.Mabao ya Mbeya City inayofundishwa na beki wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, Lipuli FC ya Iringa na Maji Maji ya Songea, Amri Said ‘Stam’ leo yamefungwa na Kelvin John sekunde ya 55 na la pili dakika ya 17 na lingine limefungwa na Mohamed Kapeta dakika ya 57.

Kwa upande wa Kagera Sugar inayofundishwa na beki wa zamani wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Mcky Mexime mabao yake yote yamefungwa na kiungo wa zamani wa Yanga, Yusuph Mhilu kwa penalti dakika ya 25 na lingine dakika ya 90 akimalizia pasi ya Nassoro Kapama.


Na bao pekee la mshambuliaji wake nyota chipukizi, Mudathir Abdlallah dakika ya 22 likatosha kuipa Coastal Union ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Singida United iliyoaliza pungufu baada ya mchezaji wak, Erick Maaibu kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 Uwanja wa Liti.

Nayo Biashara United ikaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, bao pekee la Mpapi Nassib dakika 25 Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara. 
Na bao pekee la Fully Maganga lkaipa Ruvu Shooting ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Alliance Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani.


Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na  Namungo FC ya Lindi. Salum Kihimbwa alianza kuwafungia Mtibwa Sugar akimalizia pasi ya Haroun Chanongo, kabla ya George Makang'a kuisawazishia Namungo.
Mechi nyingine tatu zilizopangwa kuchezwa leo, KMC na JKT Tanzania, Lipuli FC na Ndanda FC na Mwadu FC dhidi ya Polisi Tanzania zimeahirishwa kwa sababu ya mvua.

Post a Comment

0 Comments