BETI NASI UTAJIRIKE

RIPOTI YA MECHI: MADRID WAVUNJA MWIKO BERNABEU, RONALDO AGEUKA KOCHA


Kwa mara ya kwanza toka mwaka 2014 klabu ya Real Madrid imeibuka na ushindi dhidi ya Barcelona kwenye uwanja wake wa nyumbani Santiago Bernabeu. Real Madrid kwa kipindi cha miaka 6 hawakuwahi kushinda dhidi ya Barcelona na mara zote wamekuwa wakifungwa na kutoka sare 

Hapo jana Real Madrid walionyesha kuwa na ushindani mkali kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa wao kushinda 2-0 dhidi ya Barcelona huku mchezaji Lionel Messi akionekana si chochote kwenye mechi hiyo. 

Inasemekana kipindi cha mapumziko Ronaldo aliingia chumba cha kubadilishia nguo cha Real Madrid na aliwamotivate wachezaji wa madrid kwamba watashinda mchezo huo huku akimpa mbinu kadhaa Vinicius jinsi ya kufunga na kupitia mbinu hizo walishinda mchezo huo.

Magoli ya Real Madrid yalifungwa na Vinicius dakika ya 71 ya mchezo huku bao la pili likifungwa na Mariano dakika ya 90+5 kwenye mchezo huo. Kwa matokeo hayo Real Madrid wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Hispania wakiwa na pointi 56 mbele ya Barcelona wenye pointi 55 huku zote zikicheza michezo 26.

Kikosi cha Real Madrid : Courtois,Carvajal,Varane , Ramos ,Marcelo,Casemiro,Valverde/Vazquez,Isco/Modrick,Kroos,V.Junior na Benzema /Mariano

Kikosi cha Barcelona :Stegen,Alba,Umtiti,Pique, Semedo,Vidal/Martin,Arthur/Rakitic ,Busquet,De Jong,Lionel Messi,Griezman/Ansu Fati

Post a Comment

0 Comments