Simba SC wamezidi kuwapa raha mashabiki wao baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC katika Ligi Kuu ya England usiku wa leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck anayesaidiwa na mzawa Suleiman Matola inafikisha pointi 65 katika mchezo wa 25 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 17 zaidi ya Azam FC inayofuatia nafas ya pili.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Elly Sasii aliyesadiwa na Frank Komba na Hamisi Chang’walu wote wa Dar es Salaam, mabao yote ya Simba SC yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Msumbiji, LuÃs Jose Miquissone kipindi cha pili.
Miquissone aliye katika msimu wake wa kwanza Simba aliyojiunga nayo akitokea UD Songo ya kwao alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini alifunga bao la kwanza dakika ya 70 akimalizia pasi ya Clatous Chama
Miquissone mwenye umri wa miaka 24 aliyeibukia UD Songo mwaka 2014 kabla ya kuuzwa Mamelodi Sundowns mwaka 2018 ambayo ilimpeleka kwa mkopo Chippa United na Royal Eagles kabla ya kumrudisha Msumbiji, alifunga bao la pili dakika ya 72 akimalizia pasi ya Nahodha, mshambuliaji John Bocco.
Na baada ya kazi hiyo nzuri kocha Vandonbroeck akampumzosha Miquissone dakika ya 75 nafasi yake ikichukuliwa na kiungo wa kimataifa wa Sudan, Sharaf Eldin Shiboub.
Matokeo haya yanakuja kuelekea mechi dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga Machi 8 Uwanja wa Taifa. Yanga nayo ilishinda 2-0 dhidi ya Alliance FC ya Mwanza jana hapo hapo Uwanja wa Taifa, mabao yote yakifungwa na Ditram Nchimbi.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Hassan Dilunga/Deo Kanda dk18, Clatous Chama/Ibrahim Ajibu dk81, John Bocco, Luis Miquissone/Sharaf Eldin Shiboub dk75 na Francis Kahata,
KMC; Jonathan Nahimana, Kelvin Sospeter, Ally Ramadhani, Ismail Gambo, Sadallah Lipangile, Kenny Ally, Hassan Kabunda, Emmanuel Mvuyekule, Charles Ilamfya/Salim Aiyee dk66, Hassan Kapalata/Mohamed Samatta dk86 na Sergy Alain/James Msuva dk75.
0 Comments