BETI NASI UTAJIRIKE

RIPOTI YA MECHI: AZAM YAZIDI KUIKIMBIA YANGA KWENYE MSIMAMO WA LIGI


 Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.Mabao ya Azam F katika mchezo wake leo yote yamefungwa na mchezaji wake mpya, 

kiungo Mzimbabwe Never Tigere dakika ya 23 na 53, wakati bao pekee la Ruvu Shooting  limefungwa na Sadat Mohamed dakika ya 73.


Ushindi huo unaifanya Azam FC ifikishe pointi 54 katika mchezo wa 28, ingawa inabaki nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 68 za mechi 27. 
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ndanda SC imeibuna na ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Mabao ya Ndanda yamefungwa na Samuel John dakika ya 61 na Hussein Javu dakika ya 62, huku la Kagera Sugar likifungwa na Nassoro Kapama dakika ya 65.


Coastal Union ikaibuka na ushindi wa 2-0 dhid ya Lipuli FC, mabao ya Ayoub Lyanga dakika ya 83 kwa penalti na Hance Masoud dakika ya 90 na ushei.

Bao pekee la Peter Mapunda kwa penalti dakika ya 64 likaipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya – nayo JKT Tanzania ikaichapa Mwadui FC 1-0, bao pekee la Mohamed Rashid dakika ya 10 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Namungo FC leo imelazimshwa sare ya 1-1 na Biashara United Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Namungo ilitangulia kwa bao la Reliants Lusajo dakika ya 28, kabla ya Atupele Green kuisawazishia Biashara United 


Haya hapa matokeo ya ligi kuu Vodacom kwa mechi zilizochezwa  leo tarehe 10 



Msimamo wa ligi kuu Vodacom baada ya mechi zilizopigwa leo


Post a Comment

0 Comments