BETI NASI UTAJIRIKE

RIPOTI YA MECHI: AZAM YAENDELEA KUIFUKUZA SIMBA KIMYA KIMYA

Bao la dakika ya 90 la mshambuliajii chipukizi, Andrew Simchimba limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Kwa ushindi huo, Azam FC inayofundishwa na Mromania, Aristica Cioaba inafikisha pointi 48 baada ya kucheza mechi 25, hivyo kuendelea kushika nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 62 za mechi 24.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Namungo FC ikaibuka na ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya Lipuli FC Uwanja wa Samora mjini Iringa hivyo kufikisha pointi 46 katika mchezo wa 24 na kuendelea kukamata nafas ya tatu, mbele ya Yanga yenye pointi 41 za mechi 22.


Nayo Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbao FC, mabao ya Graham Naftal na Baraka Mtuwi Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Mwadui FC imeshinda 2-0 dhidi ya Coastal Union, mabao ya Raphael Aloba dakika ya 19 na Mussa Chambega dakika ya 82 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mtibwa Sugar nayo ikaibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Ndanda FC, mabao ya Juma Luizio dakika ya 10 na Haroun Chanongo dakika ya 85 Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro.
Biashara United 1 nayo ikaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara bao pekee la Lenny Kissu. 
Kagera Sugar ikalazimishwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba mjin Bukoba, wakati Singida United ikachapwa 1-0 na Polisi Tanzania, bao pekee la Sixtus Sabilo kwa penalti dakika ya 62 Uwanja wa Liti, zamani Namfua mkoani Singida.

Post a Comment

0 Comments