Klabu ya Real Madrid nchini Hispania imejipanga kumwaga paundi milioni 70 kunasa saini ya kipa namba moja wa Manchester United na Hispania. Mwezi Septemba 2019 De Gea mwenye umri wa miaka 29 alisaini mkataba mpya na Manchester United wenye kumuingizia kiasi cha Paundi 375,000 kwa wiki lakini Madrid wanaona ni heri wavunje mkataba kumnasa kipa huyo mwenye uwezo wa hali ya juu. Taarifa za ndani ya Manchester United zinasema kipa aliye kwa mkopo Shiffield United anategemewa kurejeshwa Old Trafford kama mbadala wa De Gea . Henderson mwenye miaka 22 anatajwa zaidi kurejea klabuni hapo msimu ujao. Historia fupi ya De Gea ndani ya United De Gea alisajiliwa na Manchester United mwaka 2011 akitokea Hispania na amecheza michezo 393 ndani ya Manchester United na mwaka 2019 alitajwa kama kipa namba moja duniani kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonyesha. Real Madrid imekuwa ikimwinda De Gea kwa muda mrefu na mwaka 2015 ilikaribia kumnasa staa huyo ila mambo hayakwenda sawa.
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments