BETI NASI UTAJIRIKE

MZAMIRU,MLIPILI NA WABRAZIL WANASUBIRI HURUMA YA SVEN KUBAKI MSIMBAZI




Ligi Kuu Bara ikiwa imesimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na hofu ya kusambaa ugonjwa wa Corona Simba ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 71 kibindoni.

Imeelezwa kuwa nyota sita ndani ya klabu ya Simba mikataba yao inakaribia kumeguka huku nafasi za wengine kubaki zikiwa mikononi mwa Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandernbroeck.

Nyota hao ni pamoja na beki mzawa Yusuph Mlipili, kiungo Hassan Dilunga na Muzamiru Yassin mshambuliaji Rashid Juma, Gerson Fraga raia wa Brazili na mwenzake Santos.

Habari zinaeleza kuwa ni Hassan Dilunga mwenye uhakika wa kuongezewa mkataba ndani ya Simba kutokana na mchango wake msimu huu ambapo ametupia mabao sita na pasi tatu za mabao.

Nafasi za nyota wawili kutoka Brazili inaeleza kuwa ni finyu nao wataungana na Wilker da Silva aliyecheza dakika tatu ndani ya Ligi Kuu Bara mbele ya Kagera Sugar.

Post a Comment

0 Comments