BETI NASI UTAJIRIKE

MWAKINYO KUREJEA ULINGONI DHIDI YA MJERUMANI

Bondia wa Super Welter Weight Mtanzania Hassan Mwakinyo Tarehe 21 Machi 2020 anashuka ulingoni nchini Ujerumani kupigana na bondia Mjerumani Jack Culcay kuwania mkanda wa ubingwa wa WBO International Super Welter Weight.

Mwakinyo,24, ambaye katika uzito wa Super Welter anashika nafasi ya kwanza kwa ubora barani Afrika  na namba 20 Duniani , atakuwa ni bondia wa kwanza Mtanzania kugombea mkanda huo ambao ni wa pili kwa ukubwa baada ya ule wa Dunia wa WBO uliokuwa unaishikiliwa na bondia Manny Pacquiao.

Mpinzani wake Jack Culcay ni bondia namba 1 kwa ubora Ujerumani kwenye uzito wa Super Welter akishika nafasi ya 4 barani ulaya.
Jack Culcay ,34, amewahi kushinda medali za dhahabu katika mashindano ya ngumi Dunia, medali ya shaba katika Olympic na kumfanya kupatiwa jina la Golden Jack na Wajerumani.
Culcay ameweza kuutetea mkanda huo anaoushikilia mara moja dhidi ya Mjerumani mwenzake Jama Saidi .

Hassan Mwakinyo akifanikiwa kushinda mkanda huu na kuutetea mara mbili atakuwa amejiweka katika nafasi ya kugombea mkanda wa Dunia ambao umewahi  kushikiliwa na Manny Paquiao.

Mwakinyo mpaka sasa amepigana mapambano 18, akishinda 16 (11 kwa KO) na kupoteza mara mbili huku Mpinzani wa wake akiwa amepigana mapambano 31, na kushinda 27 (13 kwa KO) na amepoteza mapambano manne.

Mwakinyo anaenda pigana pambano hili akiwa na rekodi nzuri ya Kushinda mapambano yake mawili ya mwisho nje ya nchi moja dhidi ya Muingereza Sam Eggington na lingine dhidi ya Muargentina Raul Ginzalenz rekodi inayombeba dhidi ya mpinzani wake.


Post a Comment

0 Comments