BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA WASHINDWA KUMLIPA MTAALAMU WA MABADILIKO, NUGAZ AFAFANUA


Uongozi wa Yanga unaendelea na mchakato wa mabadiliko ya mfumo wake wa uendeshaji kwa kufuata utaratibu uliotumiwa na moja ya timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania, La Liga imeelezwa

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuachana na Mreno Carraca Antonia Pinto ambaye makadirio ya bajeti yake yalikuwa makubwa
Katika mapendekezo yake, inaelezwa Pinto alipanga kuja nchini na wataalam takribani 30 kutoka barani Ulaya\

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz ambaye yuko karibu na mabosi wa GSM wanaosimamia mchakato huo, amethibitisha kuwa waliachana na Pinto baada ya kubaini mapendekezo yake yangewagharimu mamilioni ya fedha

"Pinto alikuwa tayari kufanya kazi na sisi lakini alitaka kuja na msululu wa watu wanaofikia 30 kutoka barani Ulaya. Tulifanya tathmini na kubaini gharama itakuwa kubwa sana hivyo tukaamua kuachana nae"
"Tunaendelea na mchakato wa kumpata mbadala wake ili aje aendeleze pale ambapo Pinto alikuwa ameanza," alisema Nugaz

Hivi karibuni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Tanzania Mhandisi Hersi Said alikuwa nchini Hispania ambapo pamoja na mambo mengine alifika klabu ya Athletic Bilbao kujifunza mambo kadhaa namna klabu hiyo inavyoendeshwa

Post a Comment

0 Comments