Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema atatumia kipindi hiki ambacho ligi imesimama kutokana na ugonjwa wa Corona kujiimarisha zaidi
Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao sita kwenye ligi msimu huu, amesema pamoja na kutekeleza program ya mazoezi aliyoachiwa na kocha wake, ataongeza mazoezi binafsi ili kuhakikisha anakuwa timamu ligi itakaporejea
Nchimbi amesema kama mchezaji mapumziko ya muda mrefu yanaweza kusababisha hata ukaongezeka uzito na baadae unaweza kushindwa kutimiza majukumu yako
"Hiki kipindi kinaweza kutuharibu wachezaji wengi kwa sababu kwanza hatupo kambini kwa maana hata kama tutaenda mazoezini tutakuwa tunatokea katika familia zetu, huku aina ya vyakula tunavyokula vinaweza kuja kutuletea madhara pale ligi itakapoendelea.
"Kama mchezaji asipokuwa makini kipindi hiki cha mwezi mzima, lazima atapata kitambi na kuongezeka uzito," alisema Nchimbi
0 Comments