BETI NASI UTAJIRIKE

MORRISON AZUNGUMZIA KUHAMIA SIMBA


Mshambuliaji wa Yanga Benard Morrison amesema ana mkataba na mabingwa hao wa kihistoria hivyo taarifa zinazomuhusisha na Simba hazina ukweli wowote
Aidha Morrison ameeleza kushangazwa upendo mwingi anaopewa na mashabiki wa Yanga kuwa hakuwahi kuona mahali popote

"Mimi nina mkataba na klabu ya Yanga, nimekuja Tanzania kwa ajili ya Yanga hivyo hizo taarifa za mimi kwenda kujiunga na Simba hazina ukweli wowote," Morrison 

"Mashabiki wa Yanga wananipa heshima kubwa, nimekuwa nikipokea zawadi kama fedha na hata chakula.Nakumbuka mchezo wangu wa kwanza Singida baada ya mchezo mashabiki walishangaza kwani walinipa fedha nyingi zinazofikia laki tano au zaidi"

"Juzi tumekwenda kucheza na Namungo, mashabiki walinipa kuku wanne.. ki ukweli upendo huu ni wa kipekee. Nimecheza Afrika Kusini, DRC lakini nakiri sikuwahi kukutana na mambo haya"

"Najihisi ni mtu mwenye deni kubwa Yanga, napaswa kufanya zaidi ili kuhakikisha naisaidia timu na kuwapa furaha mashabiki wetu ambao wamekuwa wakituunga mkono wakati wote"

Post a Comment

0 Comments