BETI NASI UTAJIRIKE

MEDDIE KAGERE AKWAMA KUCHOMOKA RWANDA



Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere anaweza kuchelewa kurejea nchini kufuatia Mashirika ya usafirishaji huko Rwanda kufuta safari zote kwa muda wa siku 30 kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa Covid-19 unaosambazwa na Virusi vya Corona.

Uongozi wa Simba ulimruhusu Kagere kurejea kwao Rwanda kwenda kumuuguza mama yake ambaye ni mgonjwa

Alitarajiwa kurejea kabla ya April 17 ambayo inatarajiwa Ligi Kuu itaendelea
Hata hivyo kwa taarifa iliyotolewa juzi, Mashirika mengi ya usafirishaji yamefuta safari zote kwa muda wa siku 30 kutokana na taarifa iliyotolewa na wizara ya afya ya nchi hiyo kufuatia kuwepo kwa ugonjwa huo

Kinara huyo wa mabao huenda akalazimika kutumia usafiri wa barabara ili kuweza kuwahi mechi zilizobaki kama TFF itabariki ligi kuendelea baada ya siku 30

Post a Comment

0 Comments