BETI NASI UTAJIRIKE

MSHAMBULIAJI NAMUNGO FC AFUNGUKA TETESI ZA KUHAMIA YANGA MSIMU UJAOmshambuliaji wa Namungo FC Relients Lusajo amesema kuwa hana tatizo na Uongozi wa Yanga iwapo watamhitaji kwani yeye ni mchezaji hachagui kambi.
Lusajo amekuwa kwenye ubora wake msimu huu akiwa na Namungo ambapo timu yake ikiwa imefunga mabao 34 amehusika kwenye mabao 14 akifunga 11 na kutoa pasi tatu za mabao.
 Lusajo amesema kuwa amekuwa akisikia kuhusu kuitwa Yanga hana mashaka na hilo kutokana na kazi yake.

"Sina chaguo na sina ubaya na Yanga kwani mimi ni mchezaji na ninaskia kwamba nahitajika na Yanga hilo mimi silijui ila kama itatokea kwangu sina hiyana.
"Iwapo Yanga wataleta ofa yao sawa nitaona inazungumza nini japo kwa sasa mkataba wangu ni dhidi ya Namungo, mchezaji hachagui kambi," amesema.

Inaelezwa kuwa Yanga inahitaji kupata mshambuliaji ili kutatua tatizo la ubutu wa safu yao ya ushambuliaji ambayo imefunga mabao 31 ikiwa imecheza 

Post a Comment

0 Comments